Vipaumbele za Tanzania na Serikali ya CCM

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Kila kitu kina sababu yake, pengine na wakati wake. Lakini kinachonituma niandike ni ukweli kwamba Tanzania imekuwa na vipaumbele kinzani sana na hali ya maisha na mambo kwa ujumla.

1. Tunapiga vita ufisadi lakini utakuta kuna watu (eti kiongozi) wanashangilia ufisadi kiaina, hawa watu wasingepata ploti ya kuishi TZ, maana kipaumbele ni kupinga vita sio kuunga mkono ufisadi.

2. Mtoto mmoja hapa TZ anakaribia kufa kisa hana laki 9 za matibabu, ugonjwa wake kazaliwa bila sehemu ya haja kubwa; Yaani hakuna hata mfumo mzuri wa kuwasaidia watu ambao wameathirika na mfumo mbaya, Anajitangaza kwenye TV kama tulufu yake ya mwisho ame afe ama asaidiwe na jamii, Serikali eti ya wananchi inachanga ghafla tu Msibani, 10milioni, Rais kasema. Inagharamia mazishi ya watu wenye uwezo mkubwa na maalufu ndani ya jamii, wanaozungukwa na mamilioni ya fedha, Waziri anapaza sauti gharama zote za serikali. Je kuhusu huyu mtoto Rais yuko kimya na Mawaziri ndo kimya cha maiti, Je kipaumbele ni nini jamani.

3. Majanga ya kitaifa utasikia rais amemtumia mkuu wa mkoa salamu za pole, tatizo kwa mtu mmoja mmoja utasikia rais atahudhuria, hivi akihudhuria anatumia mshahara wake au serikali/mlipakodi ndo analipa? na huyu mtu mmoja mmoja kwa mapenzi yake binafsi inakuwaje? utashi wa mtu na mipango ya serikali si ni vitu viwili tofauti? Maisha yanakuwa magumu bei zinakua kwa 20% mwajiri anapunguza mishahara, kipaumbele ni nin jamani?

4. Watoto wa kike anaharibika, hakuna mtu analalamikia tena kwa dhati na kuweka mkakati mahususi kuzuia hilo, Bungeni mbunge anauliza yako wapi maadili kwa wanawake kucheza uchi kwenye bendi TZ, waziri au naibu wake anajibu hawajalazimishwa hivyo hakuna shida, wao hawajalazimishwa je huoni wanalilazimisha taifa na watoto kuangalia miziki yenye watu wako nusu uchi kabisaa. waziri ktk serikali hiyo hiyo rais wake anasema unaweza ukamshitaki mtu kwa indecency (kuvaa vibaya), anawasihi waandishi wa habari wawapuuze na picha za nusu uchi, kwanini rais anaishia kwa waandishi wawapuuze, hawezi kuchua hatua kama kipaumbele cha taifa kwanza, furaha za mtu, pesa na mali baadaye? unavunja maadili ya nchi na taifa eti unatafuta kipato/maslahi waziri na rais wanakuwa hawana la kufanya, kweli kipaumbele TZ ni nini?

Naomba kuwasilisha, waTZ tuambiane kipaumbele ni NINI Tanzania na Serikali yake?
 
Orodhesha vipaumbele unavyodhani vinakinzana ili tuvijadili! Ulichokifanya ni kutoa mifano.
 
Back
Top Bottom