Vipa-unyuma vya mgombea wangu/ sorry vipaumbele vya thithiem 2010-2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipa-unyuma vya mgombea wangu/ sorry vipaumbele vya thithiem 2010-2015

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elli, Jun 22, 2010.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  haya, haya sasa wadau, kipyenga ndo hiiichoo kimepulizwa, kama hujamaliza kibanda chako hapa ndo penyewe mwana. Jana kiranja mkuu alikuwa akichukua fomu kulee kwa ajili ile ileeee. Nilitamani sana niangalie japo kwa robo sekunde lakini bosi wangu alikataa kata kata, kwa madai kuwa nilikua nataka kugoma na yeye tayari alikuwa na power ya kuni-fire nje ya hili li-ajira linaloniwezesha kupanda daladala na kukesha kwene folen hadi kulala na kupunguza upepo..​

  Leo, nikajihimu asubuhi nipate gazeti moja ambalo liliandika kwa mbwembwe kweli, haya tuone sasa....mmmhhh, vilio, vioja, na masikitiko matupu. Walaah naapa hakuna jipya, ooh sorry simlaumu kumbe alisema ILANI huwa inaandaliwa na chama na hadi anaenda kuchukua fomu Sisi na Emy walikuwa hawajaanaa bado.​

  Wadau, nimelazimika leo kuwaandikia waraka huu mfupi ili hasa nijue kuwa mwaka mwingine wa mavuno ufikapo, tutakula au ni nyani ndiye atakayefaidi, kwa mtazamo wangu, nashindwa kuelewa maana ya neno vipaumbele ( priorities) kwa hawa mapacha walioungana a.k.a Siisii na Emy. Ninavyofikiri hivi ni vipa-UNYUMA au vipangamizi vya maendeleo labda au pengine setbacks za wajumbe hawa wa kufikirika. Hebu soma haka ka-verse hapa​

  JK aboresha kaulimbiu, AJA NA ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI

  Hivi, Ari zaidi ya kutufanya nini? Nguvu zaidi ya nini? na Kasi zaidi ya kuelekea wapi? Kuzimu, ahela au wapi? Kasi ya kuongeza malalamiko ya wafanyakazi na vizazi vyao? Ndo maana nasema , kama huna kibanda kiwa mjinga mwaka huu hutakimaliza, mwenzenu JK ndo huyooo anataka amalizie kile Kijiji chake pale mble ya Chalinze mzee bara bara ya kuelekea Tanga/Kilimanjaro.

  Kwa kifupi, hapa hakuna vipaumbele ila sasa maneno yamewaishia kama vile mtu aliyeko ukweni anavyoshikwa na haja na kushindwa kwenda kulee, kunako mambo.​

  Vipa-unyuma vyetu vidumu daima.​

  Mimi wako Shemdodo Original.​
   
Loading...