Viongozi wetu wa dini acheni unafiki

saimon111

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,736
1,352
Wanajamvi kwanza napenda kuwatakia heri ya pasaka.....

Nimewaza sana inamaana viongozi wetu wa dini walikua hawaelewi uchaguzi wa Zanzibar ulikumbwa na wingu lipi mara ya kwanza mpaka ukatangazwa kubatirishwa ?

Sasa kama walikua wanajua ni uchaguzi batili, swali langu ni je kwanini viongozi wa dini walishiriki kuuapisha uongozi huo kuingia madarakani tena kwa kushika vitabu vitakatifu vya dini ambavyo vinakataza dhuluma pamoja na unafiki....? Au viongozi wetu nao ni wamoja wao ?

Mpaka uchaguzi wa TZA visiwani unarudiwa hatujasikia kiongozi yeyote wa dini aliyenyanyua mdomo na kukemea dhuluma zilizoendelea as if hawakua wanaona kinachoendelea
 
Viongozi wa dini ndio waliomsulubisha Yesu.

Viongozi wa dini ndio waliouwa mitume na manabii.

Hakuna jipya chini ya jua, yote yalikuwepo na yatapita, na yatakuja mapya ambayo nayo yalikwisha kuwepo kabla
 
Ni wanafiki sana na wananjaaa sana kumbuka wale walikuwa bunge la katiba ndo ujue ni nikitu cha kujifichia tuuu
 
Viongozi wa dini wa Tanzania hasa madhehebu makubwa ni wanafiki sana Hata maandiko matakatifu yanahubiri kwanza Haki kisha Amani lakini viongozi hao wanaubiri Amani ,Haki hawahubiri Kwa sababu wanajua toka mioyoni mwao kuwa Nchi hii hakuna HAKI kuna AMANI TU
 
.....wanaogopa ile mikwara ya wauza unga wanaojificha makanisani watatumbuliwa, bila kusahau mtego wa misamaha ya kodi, wakichomoka kwenye hii ndoano basi wao ni wanadini kwelikweli...
 
Mnawaweka katika wakati mgumu. Wao wanatoa mafundisho lkn si kulazimisha watu watekeleze. Wakikomaa sn tutarud hapa kuwaponda kuwa wanachanganya dini na siasa. Na ukumbuke kuwa kiongoz wa dini akishupalia hoja fulan na waumini wake wakifuata imani nyingine hawata kubali. Hapo sasa unatokea mgawanyiko mtaacha siasa mtaanza mgogoro wa kidini. Hao wanasiasa nao ni waumini pia katka dini zao km ni dhambi wanajua kuwa wanatenda dhambi. lkn kama ilivyo kwa wazinzi na wenye kukufuru na wanasiasa wanajijua kabisa kuwa ni WAUAJI, WAONGO, WANAFIKI, WEZI, WALAGHAI, MATAPELI, WALAFI, WALA RUSHWA, MAFISADI nk kiongozi wa dini alishatoa mafundisho na maonyo lkn hawezi kumzuia mtu kutenda dhambi.
 
Kuna wakati mwingine kama kiongozi wa dini lazima utumie Busara na Hekima ili kunusuru taifa katika kuingia kwenye machafuko unadhani viongozi wa dini na wao wangetia chachu kidogo tu na walivyo na waumini wengi nchi hii leo ungeweza kukaa hapa na kupost...Hali ilikuwa tete mno ilikuwa inasubir mtu mmoja awashe njiti tu maana petrol ilikuwa ishamwagwa na imesambaa kila mahali..
 
Wanajamvi kwanza napenda kuwatakia heri ya pasaka.....

Nimewaza sana inamaana viongozi wetu wa dini walikua hawaelewi uchaguzi wa Zanzibar ulikumbwa na wingu lipi mara ya kwanza mpaka ukatangazwa kubatirishwa ?

Sasa kama walikua wanajua ni uchaguzi batili, swali langu ni je kwanini viongozi wa dini walishiriki kuuapisha uongozi huo kuingia madarakani tena kwa kushika vitabu vitakatifu vya dini ambavyo vinakataza dhuluma pamoja na unafiki....? Au viongozi wetu nao ni wamoja wao ?

Mpaka uchaguzi wa TZA visiwani unarudiwa hatujasikia kiongozi yeyote wa dini aliyenyanyua mdomo na kukemea dhuluma zilizoendelea as if hawakua wanaona kinachoendelea
Hapa mjini Dini biashara, kila nyumba 15 kanisa.. ina maana dili inalipa
 
NIMESIKIA KWENYE MEDIA ETI ASKOFU MMOJA AMESEMA KUCHAGULIWA SHEIN NI MPAGO WA MUNGU!
 
Mnawaweka katika wakati mgumu. Wao wanatoa mafundisho lkn si kulazimisha watu watekeleze. Wakikomaa sn tutarud hapa kuwaponda kuwa wanachanganya dini na siasa. Na ukumbuke kuwa kiongoz wa dini akishupalia hoja fulan na waumini wake wakifuata imani nyingine hawata kubali. Hapo sasa unatokea mgawanyiko mtaacha siasa mtaanza mgogoro wa kidini. Hao wanasiasa nao ni waumini pia katka dini zao km ni dhambi wanajua kuwa wanatenda dhambi. lkn kama ilivyo kwa wazinzi na wenye kukufuru na wanasiasa wanajijua kabisa kuwa ni WAUAJI, WAONGO, WANAFIKI, WEZI, WALAGHAI, MATAPELI, WALAFI, WALA RUSHWA, MAFISADI nk kiongozi wa dini alishatoa mafundisho na maonyo lkn hawezi kumzuia mtu kutenda dhambi.
Hatusemi wasiwaapishe kwa maana kufanya hivyo kutahatarisha maisha yao na uhai wa madhehebu yao. Ila wangetumia lugha rahisi ya lakini siyo za kuremba hadi kuwa chukizo mbele ya Mungu. Maana aliyesikiliza zile dua kwa umakini atagundua unafiki uliokithiri wa watu hawa kunakonajisi imani zote zinazoamini Mungu hadhihakiwi.
Udhaifu huu ulionyeshwa na wote, waislamu na wakristu!
Ila jambo moja linanifariji; kiapo kitabaki batili kikiwa batili mbele za Mungu hata kikiombewa na maimamu na maaskofu wa dunia nzima!
 
Siyo wanafiki tu bali wanafiki waliotukuka. Wao wanawasiliana na Mungu baada ya uchaguzi au kabla? Wanajuaje kuwa aliyechaguliwa ni chaguo la Mungu hata kama ushindi wake umejaa kasoro na wizi? Waache kutuenjoy na siku si nyingi nyumba za ibada zitabaki tupu kwa waumini kutokuwaamini tena.
 
Mimi cmo. Ila kumbuka hawa nao ni wanadamu na wanamapungufu yao.
 
Hivi huyu anasema Dini ni biashara kwa kuwa kila baada ya nyumba 15 unakuta kanisa....mbona hawazi kila baada ya nyumba 2 ni Bar?
 
Back
Top Bottom