Viongozi wetu Tanzania tunawapataje?

Oct 7, 2019
51
156
Kuanzia 2017 niliandika Sana kuhusu aina ya Viongozi tunaowahitaji. Makala zangu asilimia tisini nililenga kuandaa watu kutambua aina ya Viongozi Bora hata kwa kuiga Kutoka mataifa yaliyoendelea.

Kwa upande wangu nafikiri nilimaliza kabisa kila kitu katika kutoa Elimu ya Nini tufanye ili rasilimali zitunufaishe.

Narudia tu kwa makusudi Kuna watu huwa hawaelewi mpaka SoMo lirudiwe rudiwe.

Hiyo picha Hapo ni Zhang Weiwei ni Director Katika chuo kikuu cha Fudah University China. Anaelezea ni kwa namna gani china inapata viongozi wake wa kisiasa.

Aliwahi kusema viongozi wote wa China lazma wapitie mchakato unaojulikana kama Selection plus Election. Yaani kabla ya kuwa kiongozi china lazma mchakato wa kuwachuja ufanyike kwa kuangalia ulishawahi kufanya nini kabla.

Maeneo muhimu wanayoangalia ni uwezo wako wa kupambana na Umaskini, uwezo wako wa kutengeneza Ajira, uwezo wako wa kuyatunza Mazingira na uwezo wako katika local economic Growth.

Wanawapima toka wakiwa huku chini yaani ngazi za chini kwenye Clip hii anadai viongozi Sita kati ya saba ambao ni Top kabisa katika Serikali yao wamepitia mchakato huo na wamepimwa toka wakiwa katika ngazi za Chini za Kiuongozi.
Wao wachina wanacriticize mfumo wa Westerns ambao mtu anatokea from nowhere anakuwa kiongozi.

Hapa anatoa mfano kuwa Kama Trump na Bush wangepitia mfumo wa selection na election kamwe wasingelikuwa Viongozi kwa kuwa mfumo huo ungewatema na wasingelifikia kuwa Viongozi.

Suala la kuandaa Viongozi China huchukuwa muda Kuna hatua tano ambazo utapitia katika kipindi fulani Cha muda ukifanyiwa assessment hatua ya kwanza huitwa analysis and proposal, hatua ya Pili huitwa democratic recommendation, hatua ya tatu huitwa appraisal, hatua ya nne huitwa discussion and decision na hatua ya Mwisho ni appointment.

Katika hili wachina wao hutumia msemo wao maarufu kuwa "It takes seven years to see if a tree can grow into suitable building materials." Kwa maana ya kuwa huchukua miaka Saba kugundua Kama mti flani unaweza kutumika kwenye ujenzi.

Pamoja na hayo kila mtumishi pale China ambaye ni mtumishi wa umma haingilii dirishani tu Kama hapa kwetu wanavyofanya bali lazima ufanye mtihani wa utumishi wa Umma unaojulikana Kama "KEJU".

Keju ni mtihani ambao kimuondo huwa na maswali 135 multiple choice na maswali Mengine ya kujieleza. Mtihani huo hujumuisha hesabu, Lugha, world affairs na Logic, uwezo wa kusoma, psychological potentials, uwezo wa kutatua matatizo nk.

Hapa hata Viongozi wa Umma lazima wafanye mtihani huu, huwezi kuwa kiongozi Kama cv yako haionyeshi kuwa uliwahi kufanya KEJU na ukafaulu.

TANZANIA.
Sarakasi za kura za maoni Mmeziona? Sitaki kuongelea Sana eneo hili....lakini itoshe tu kusema kuwa niliwahi kusema Kuna umuhimu wa CCM kumsadia Rais kupata wabunge wenye uwezo na kuachana na wale aliorithi toka awamu nyinginezo.

Nilitahadharisha kuwa tumerahisisha mno Ubunge wetu, yaani eneo muhimu kama bunge tunapeleka mtu ni mtu hili kosa kubwa na hatutokaa tuendelee tutabaki kuzisifia nchi nyingine duniani.
Tanzania ili uwe kiongozi unatakiwa uwe:-

1. Aidha una fedha za kuhonga Wapiga kura...

2. Aidha unajua Sana kusifia mamlaka na kulamba soli.

3. Aidha wewe una ndugu au connection na wenye mamlaka.

Kwa style hii tusahau maendeleo.... Hakuna ubunifu na ndio maana zoezi la kutumbua ni endelevu hapa nchini.

Wanaopewa madaraka nchini wamepimwa? Waliwahi kufanya Nini hapo kabla?

Haya maswali tuwaachie wazee wa vetting ambao ndio wenye jukumu la kukusanya taarifa za watu kabla ya kuwa Viongozi.

109455681_4158716117502927_2070652964870837040_n.jpg
 
Back
Top Bottom