Viongozi wetu na PHD zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wetu na PHD zao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Big Dady, Aug 18, 2010.

 1. B

  Big Dady Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Miaka ya karibuni kumeibuka watanzania na hususani viongozi wetu kujinadi kwa PHD zao. Inaelezwa kwamba baadhi yao wana PHD feki maana zinapatikana kutoka vyuo ambavyo havitambulikani kitaaluma. Kubwa zaidi ni kuibuka kwa watunikiwa wengi wenye PHD za heshima. Hao ndio kabisaaa, hupenda kujionesha kama watu waliobobea wakati hakuna cha maana waliochozamia hadi kupata shahada hizo, 'SHAHADA ZA UZAMIVU'. Rafiki yangu mmoja alinieleza kwamba mmoja wa wazamivu hao alikuwa akiita PHD kama 'Push Heaven Down'.

  Lakini tofauti na viongozi wetu wanavyojinafasi hapa na PHD hizo, hali ni tofauti kwa nchi za wenzetu wa Ulaya. Kwa taarifa nilizonazo kutoka vyanzo mbalimbali ni kwamba viongozi kama Bill Clinton, Tony Blair, Al Gore, Michael Gorbachev, David Cameron, na hata Barack Obama aidha ni madaktari au maprofesa wa kitaaluma lakini hata siku moja huwezi sikia wakijiita hivyo. Hao ni mfano wa viongozi wengi wa nchi za magharibi ambao mara wanapoingia kwenye siasa, vyeo vya kitaaluma huachana navyo.

  Sasa vituko vya uswahilini hapa kwetu, kila kiongozi anataka atambulike kama dokta, ndio kuna dr. Kikwete, dr. Shein, dr. Karume, dr.kifimbocheza, n.k. Ukiacha d. Shein, hawa wengine hawana taaluma yoyote ya kustahili kupewa PHD, ila kwa kupenda sifa wanadhani kuitwa dokta ni ujiko sana. Amani Karume hadi anapata Urais wa zanzibar alikuwa hana hata digrii (shahada) moja, alikuwa just F 6 leaver, leo hii eti dokta. Tunawaomba msiringie sana PHD za kupewa. Kama ninyi ni majasiri si mwende shule kama Dr. Magufuli ambaye kila mmoja aliona akipewa PHD yake. Acheni kutuzuga na PHD za mezani.

  Mwisho, nampongeza sana Benjamini Mkapa (rais mtaafu) ambaye alikataa kujiita hivyo baada ya kutunikiwa PHD ya heshima. Huyu ni mfano wa viongozi wa kijamii. Nakumbuka alikataa kuitwa mtukufu mara baada ya kuapishwa kuwa rais. Hii imekuwa nzuri maana bila hivyo huyu Rias wa sasa mpenda sifa kabisa angependa apate utukufu wote.
   
Loading...