Viongozi waungwana na wa kuigwa katika picha

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,109
18,326
Kwa kweli tuna lakujifunza, kwa viongozi hawa wanao tambua kwamba wana wajibu wa kutuongoza katika mapambano ya corona.

Nilikua na mtu mmoja hapa, akaniambia nisiwe na hofu yoyote, baada ya kumwuliza hofu ya nini akaniambia kwa sasa Tanzania ina hofu ya aina 2.

1. Wale wanaosema hawana hofu na corona wanawahofia wanadamu wengine.

2. Wale wanaosema hawawahofii wanadamu wengine, wanahofu ya corona.

Je, hofu ni mbaya juu ya jambo hatari?

Tuvae mask (barakoa) kwa maisha yetu na ya wengine wanao tuzunguka.

IMG_20210219_115430.jpeg
FB_IMG_1613728353981.jpeg
IMG_20210219_115517.jpeg
IMG_20210219_115150.jpeg
IMG_20210219_095934.jpeg
IMG_20210218_134104.jpeg
 
Hizi danganya toto za kumsingizia Mungu kila kukicha zitakwenda na watu wengi sana , watumishi wa Mungu ndiyo askari wa mbele kwenye mambo ya kiroho na wamevaa barakoa, ila kuna watu bado hawaelewi angalau hizo barakoa zinaweza kupunguza maambukizi wao kila kukicha Mungu atafanya miujiza 🙄.
 
Nimekuwa mwaminifu wa kuvaa barako, cha ajabu ninawiki mbili uraiani nikitokea kuugua Corona!!

Labda niseme hivi, Corona ipo na inauwa, tujikinge katika Hali zote, Ila tusisahau hili, Aspotulinda Mungu tutajipa shiida Sana kuzijaribu akili zetu na uwezo wetu eti tutasalimika Kwa sababu tumejidhatiti kujilinda Kwa kila njia

Mungu asipoulinda mji, wakeshao wakesha bile
 
Hizi danganya toto za kumsingizia Mungu kila kukicha zitakwenda na watu wengi sana , watumishi wa Mungu ndiyo askari wa mbele kwenye mambo ya kiroho na wamevaa barakoa, ila kuna watu bado hawaelewi angalau hizo barakoa zinaweza kupunguza maambukizi wao kila kukicha Mungu atafanya miujiza .
Kwanza usimkufulu Mungu Kuna siku utamwitaji. pili kifo akikwepeki marekani anafwata taratibu zote lakini Nini kinaendelea
 
Mkuu ubarikiwe sana
 
1. Sanitize
2. Nawa mikono
3. Usizurule ovyo bila sababu kwenye misongamano

4. Vaa barakoa

Serikali kazi yake ni kuhimiza wanachi wafuate taratibu za kiafya.

Mbona watu wanatumia kondom kujikinga na ukimwi, kwanini tusivae barakoa?

Mungu hajatupa akili kama matope, bali ametupa akili zitusaidie katika.maisha na akili ikikoma basi tumwachie Mungu.

Lakini kula bila kunawa kisha unamsingizia Mungu kwamba atakulinda na kipindupindu sahau.
Mimi nashauri tuvae mavazi kama Yale ya madaktari ya kujilinda na Corona au magunia .
Barakoa peke yake HAZITOSHI.
 
Kwanza usimkufulu Mungu Kuna siku utamwitaji. pili kifo akikwepeki marekani anafwata taratibu zote lakini Nini kinaendelea
Jinga kabisa wewe, natafuta kitufe cha kukupiga block sikioni, lini Wizara yako ya Tangawizi na kujifukiza ilitoa takwimu za waliokufa. Chizi wahedi wewe
 
Unafananisha vipi Corona na ukimwi kwenye kujilinda?.
Ukimwi mpaka ufanye ngono .ILA Corona hata ukigusa kitu kilichoshikwa na muathirika wa Corona unayo hata kama umevaa barakoa.
Sasa hapo barakoa imekusaidia nini?
1. Sanitize
2. Nawa mikono
3. Usizurule ovyo bila sababu kwenye misongamano

4. Vaa barakoa

Serikali kazi yake ni kuhimiza wanachi wafuate taratibu za kiafya.

Mbona watu wanatumia kondom kujikinga na ukimwi, kwanini tusivae barakoa?

Mungu hajatupa akili kama matope, bali ametupa akili zitusaidie katika.maisha na akili ikikoma basi tumwachie Mungu.

Lakini kula bila kunawa kisha unamsingizia Mungu kwamba atakulinda na kipindupindu sahau.
 
Hizi danganya toto za kumsingizia Mungu kila kukicha zitakwenda na watu wengi sana , watumishi wa Mungu ndiyo askari wa mbele kwenye mambo ya kiroho na wamevaa barakoa, ila kuna watu bado hawaelewi angalau hizo barakoa zinaweza kupunguza maambukizi wao kila kukicha Mungu atafanya miujiza .
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anasingiziwa tu. Kwanza hayupo.

Anayebisha athibitishe Mungu huyo yupo.
 
Back
Top Bottom