Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,706
- 149,945
Raisi Magufuli,kama kweli umeamua kutenda haki,katika Bunge lijalo serikali yako ipeleke mswaada wa marekebisho wa malipo ya kustaafu(pensheni) kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa(Raisi,Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu) ambao wako entitled kulipwa 80 % ya mshahara wa kiongozi alieko madarakani kwa mujibu wa sheria iliyopo.Hii haikubaliki hata kidogo.
Pia,malipo ya mafao kwa wabunge kwa kipindi cha miaka mitano nayo yamekuwa yakitajwa kuwa ni makubwa kulinganisha na yale wanayolipwa watumishi wengine wa umma wanaofanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30 huku mbunge anaefanya kazi kwa miaka 5 tu analipwa kiasi kikibwa cha fedha kumzidi mtumishi huyo.
Waandishi wa habari,leo baadhi yenu kwenye kurasa za mbele za magazeti yenu mmeanika mishahara ya ma-CEO wa Taasisi mbalimbali za umma,kwa moyo huo huo,naomba kesho katika kurasa zenu za mbele mtutajie mishahara ya ya viongozi hawa wakuu wa kitaifa na pensheni wanazopata viongozi wastaafu.
Baada ya hapo,tuwekeni malipo ya mafao ya wabunge kwa muda wa miaka mitano ya utumishi wao na kisha mtoe mlinganisho wa mafao anayopata mtumishi wa kima cha chini au hata yule anaepata kima cha kati kwa miaka zaidi ya 30 anayofanya kazi serikalini.
Tusipokuwa makini na tukabaki kuwa watu wa kushangilia tu pasipo kuhoji,kuna hatari ya kuongezeka kwa "gap" baina ya wanasiasa na watumishi wengine wa umma katika nchi hii.
Jambo lingine la kutazama ni kuwepo kwa madai ya wajumbe wa bodi kwa baadhi ya mashirika ya umma kulipwa posho kubwa kupindukia za vikao vya bodi.Hili nalo lichunguze na kisha uchukue hatua kukomesha huu ubadhirifu uliohalalishwa kisheria.
Raisi Magufuli haya yakikushinda bora uwaache hao ma-CEO waendelee kulipwa hiyo mishahara maana hakuna unachookoa kama utaacha kupunguza malipo haya ya wanasiasa na uwambie waziwazi hao wabunge kuwa wakigoma kupitisha miswaada hiyo unalivunja Bunge turudi kwenye uchaguzi.
Raisi, tenda haki kwa kusimamia/kufanya mambo "tangible" na sio tu kupunguza mshahara wa hao ma-CEO ambao wanahesabika na huwezi okoa hata zaidi milioni 200 kwa ku-deal na hao tu na kuacha wanasiasa wenzako wanaotafuna mabilioni ya walipa kodi kwa stahiki za kujipendelea.