Viongozi wakubwa waliofariki dunia wakiwa madarakani barani Afrika

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,271
2,401
PhotoCollage_1617638843221.jpg
Sina hakika huu wimbo ni wa lini, ila kwa video nimeona kama ni wa kipindi kile cha ajali ya wale watoto wa sekondari Arusha. Pamoja na hayo, hiyo sio mada yenyewe.

Umetokea msiba wa Rais Magufuli (Mungu amrehemu) ndipo nausikia huu wimbo rasmi. Nimeendelea kuusikia kupitia kituo changu pendwa u fm.

Jana kwa mfano ulirudiwa kwa saa mbili hivi mfululizo. Kifupi ni kwamba hauchoshi. Bado hiyo sio stori.

Tangu nianze kuusikia huu wimbo, nimekuwa nikiutafuta bila kufanikiwa, hasa youtube. Pengine nilikuwa nakosea kuutafuta kwa kutokujua jina lake. Nikajaribu hadi shazam bila mafanikio. Sababu yote hiyo kuna kitu nilikuwa nakitafuta. Sauti ya nani?
Kwa kweli nilipofika kwenye maneno haya:
Asubuhi ilikucha sawa
Amani ilikwepo sawa
Nilikwona ukienda
Lakini hukurejea, ah...

Nafsi yangu ilikataa kutulia. Ni nsni huyu mwenye hii sauti ya ajabu? Sauti iliyotulizwa. Sauti yenye ufundi katika kuimba. Nilibaki na maswali mengi sana.
Nilijaribu kupachika hapo waimbaji ninaowajua ila sikupata jibu. Nilibakia na kiu kubwa sana

Nilivuta picha akilini kuwa lazima kwa sauti ila atakuwa 'full package' tu! Basi nikabaki kuwa msikilizaji. Na u fm kama walijua kuna watu wanavutiwa na huu wimbo. Actually haukuwa wimbo pekee uliorudiwa kwa wakati mmoja mara nyingi, ila jana ilikuwa funga kazi.

Jana hiyo wakati wimbo ukiebdelea nikachukua tena simu yangu, huyoo youtube. Mara nikaona jina 'Ni Salama'. Kuplay ikaja ile sauti ninayoisikiaga, yaani yule mwimbaji wa kwanza, nikasema Yes!

Mara namwona Miriam Lukindo. Nilistaajabu sana. Awali nimeshasikia baadhi ya nyimbo zake ila sikuwahi kumkubali namna hii. Nilimwona Clouds akitambulisha wimbo wake fulani uliochangamka hivi ila sikuona maajabu katika vocals.

Nikamwona tena katika kipindi kingine Clouds akihojiwa kisha akaimba live. Nikaona anaimba vizuri. Awali nilikuwa sceptical kuwa kisa Dr. Mauki (mumewe) mtu maarufu basi anatembelea nyota ya Mister.

Sasa katika wimbo huu hakika umeonesha maajabu. Umebarikiwa sauti tulivu. Habari njema zaidi unajua kucheza nayo. Barikiwa sana. Aina ya nyimbo zinazokufaa na kuonesha uwezo wako ni zile zilizotulia.
Kundi lenu kwa kweli mlijichagua, na ujumbe katika wimbo umeshiba.
Hakika 'Ni Salama' utabaki kuwa wimbo wangu wa wakati wote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom