Viongozi wa UVCCM Arusha watwangwana makonde leo

Antar bin Shaddad

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
202
101
kikao cha kamati ya utekelezaji ya UV-CCM mkoa wa Arusha kimevunjika leo baada ya wajumbe wawili Mrisho Gambo na mwenyekiti wa UV-CCM wilaya Karatu Bayo kutiana makonde kavukavu na baadaye mwenyekiti kutiwa mbaroni na polisi.

Wajumbe hao walizipiga kavukavu baada ya mkti huyo wa karatu kujaribu kumzuia Gambo kwa madai kuwa si mjumbe halali wa kikao hicho kilichokuwa kinaoongozwa na kaimu Mwenyekiti Esther Maleko ambaye alikaimishwa na Mwenyekiti James Ole Millya.

Baada ya vurugu hizo kikao kilivunjika na na Mwenyekit huyo alikamatwa na polisi na hadi majira ya saa mbili usiku alikuwa bado yuko mahabusu ya kituo kikuu cha polisi mjini Arusha

Awali kabla kuibuka kwa vurugu wajumbe walilazimika kupiga simu kwa Katibu Mkuu wa UV-CCM Martine Shigela kuuliza uhalali wa Gambo kushiriki kikao hicho na Shigela aliwajibu kuwa hakuna kikao chochote kilichiowahi kumsimamisha Gambo hivyo ni mjumbe halali na kutokana na majibu hayo ndipo Mwenyekiti wa Karatu alipoamua kujichukulia sheria mkononi kujaribu kumtoa Gambo kwa nguvu ndani ya kikao.

Chanzo cha kumtoa Gambo inaelezwa kuwa ni hatua ya mjumbe huyo kukataa kuungana na kundi la vijana wa arusha wakioongozwa na Millya ambao wamenunuliwa kumfanyia kammpeni Lowassa katika harakati za kuwania Urais 2015.Nawasilisha
 
Haiingii akilini....please tuletee source ya hii taarifa bana!

"wamenunuliwa kumfanyia kammpeni Lowassa katika harakati za kuwania Urais 2015"

Kwani huyu ameshatangaza kugombea au?
 
Wanauana wao kwa wao, hawa nawafanaisha na wale waasi wa Libya ambao sasa hivi wanageukana wao kwa wao
 
shauri yao, kupigana hadharani ni jinai, polisi wamefanya kazi yo, lakini hitajulikana kuwa ni kazio mpaka mahakama imtie adabu mhusika wa ugomvi
 
Subirini mengi kwenye uchaguzi wa hiki chama mwaka huu,watatoana roho kabisa..hii ni rasharasha tu,mafuriko yanakuja.
 
Haiingii akilini....please tuletee source ya hii taarifa bana!

"wamenunuliwa kumfanyia kammpeni Lowassa katika harakati za kuwania Urais 2015"

Kwani huyu ameshatangaza kugombea au?

You can't be as stupid as you'd want us to believe!
 
Haiingii akilini....please tuletee source ya hii taarifa bana!

"wamenunuliwa kumfanyia kammpeni Lowassa katika harakati za kuwania Urais 2015"

Kwani huyu ameshatangaza kugombea au?
ndiyo,huyu ameshatangaza kugombea
 
Haiingii akilini....please tuletee source ya hii taarifa bana!

"wamenunuliwa kumfanyia kammpeni Lowassa katika harakati za kuwania Urais 2015"

Kwani huyu ameshatangaza kugombea au?

Unaishi dunia gani wewe
OTIS
 
Haiingii akilini....please tuletee source ya hii taarifa bana!

"wamenunuliwa kumfanyia kammpeni Lowassa katika harakati za kuwania Urais 2015"

Kwani huyu ameshatangaza kugombea au?

Hii hbari ilianza vizuri mashaka yameanza baada ya kusema vijana wa kumpigia kampeni Lowasa??? Kivipi?
 
Mimi simtetei Lowassa lakini you can't prove that amewanunua na kama unaweza tuletee ushahidi hapa siyo kukurupuka tu, na huko kutangaza kwamba anagombea ni lini alisema hivyo? Mods hii habari ilitakiwa ipelekwe jukwaa la tetesi siyo hapa bana!
 
Haiingii akilini....please tuletee source ya hii taarifa bana!

"wamenunuliwa kumfanyia kammpeni Lowassa katika harakati za kuwania Urais 2015"

Kwani huyu ameshatangaza kugombea au?

Kama haiingii akilini kwako kwa wengine bado ina make sense.
 
Mimi simtetei Lowassa lakini you can't prove that amewanunua na kama unaweza tuletee ushahidi hapa siyo kukurupuka tu, na huko kutangaza kwamba anagombea ni lini alisema hivyo? Mods hii habari ilitakiwa ipelekwe jukwaa la tetesi siyo hapa bana!
Mtu utajua kajinyea si mpaka uone kinyesi bali harufu ya kinyesi inakufanya uhisi kuwa huyu mtu kajinyea,mnaotaka ushahidi nendeni kwenye harambee za makanisa ndio mjue mtu anataka uraisi,msitake kutuletea za hakunaga hapa wakati siri i wazi,si watu walikubaliana kuwa wataachiana uongozi(wamefanya uongozi haki yao)au nalo hamlijui acheni uzushi
 
Haiingii akilini....please tuletee source ya hii taarifa bana!

"wamenunuliwa kumfanyia kammpeni Lowassa katika harakati za kuwania Urais 2015"

Kwani huyu ameshatangaza kugombea au?

Source?
Yanini wakati yeye mwenyewe yuko mahala pa tukio?

Ama unafikiri wote wanaotumikia mafisadi wanapenda?
Wengi wako pale kwa sababu ya habari iwafikie wanainchi wapenda nchi yao kama hivi sasa

Raia wameshawachoka magamba kitambo.

Eti lete source maana hbr hii hainiingi,kweli wee ni gamba flu!
Habari ndiyo hiyo!
 
Back
Top Bottom