mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Kwamba viongozi wa upinzani wanafanya biashara ya dawa za kulevya, inawezekana. Kanuni za kuichunguzi zinasema hakuna muhalifu wala asiye muhalifu hadi uchunguzi utakapokamilika.
Lakini lazima ufikirie sana usiwe bwege! Serikali ya CCM imekuwa madarakani kwa kipindi kirefu ikiendesha siasa za chuki na fitina dhidi ya wapinzani. Sasa kama viongozi wa upinzani wamekuwa wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya, basi ujue walishirikiana moja kwa moja, bega kwa bega na viongozi wa dola. Haingewezekana kuingiza, kusambaza, kusafirisha nje ya nchi bila ulinzi wa mkono wa dola.
Na katika nadharia hiyo, dola ndio inakuwa boss wa biashara hiyo, au labda tukubaliane kuwa hakukuwa na dola. Maana yake hawa akina Kamanda Sirro, na Mstaafu Nzowa na wenzao walikuwa wapowapo tu, au nao walishiriki? Tafakari tu! Kwamba kiongozi wa upinzani katika nchi yenye siasa za kikuda kama Tz afanye biashara hii haramu halafu abaki salama hadi leo!
Fikiria sana usiwe bwege kijana.