Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,335
- 13,293
Haipiti wiki mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu kutoka SMZ kutembelea Dar kikazi au kibinafsi! Kwa kuwa serikali ya SMZ haijawatafutia nyumba za kuishi viongozi hao wawapo Dar hulazimika kukaa katika hoteli kubwa kubwa! Gharama za viongoz hawa kuishi hotelini ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi wa Zanzibar.
Chukulia mfano wa Maalim Sefu tangu atoke hospitalini Hindu Mandal amekuwa akiishi hoteli ya Serena.
Kwa mujibu wa chumba anachoishi kiongozi huyo chenye hadhi ya rais ambacho hutozwa kwa Dola za Marekani 2,801.50, ambapo dola moja ni sawa na Sh 2,180. Hivyo kwa siku saba hadi kufikia leo Serikali imemlipia Maalim Seif, Sh milioni 42.946.
“Magufuli (Rais), alipokwenda kumwona alimuuliza ni nani anayemlipia gharama za hoteli na Maalim alisema wazi ni SMZ, lakini ninachotaka kuwaambia Maalim Seif hana nyumba Dar es Salaam.
“… kama wapo viongozi waliopewa nyumba wa SMZ ni hao lakini si Maalim Seif, tangu mwaka 2010 hana nyumba na hufikia hotelini, hana nyumba ya Serikali wala yake binafsi,” alisema Hamad.
Alisema pamoja na hali hiyo kwa sasa Serikali ya Muungano ndiyo inayolipa gharama za Maalim Seif kuishi hotelini kwa agizo la Rais Dk. John Magufuli.
Alisema ahadi ya Rais Magufuli ya kusaidia kulipia hoteli anayoishi Maalim Seif inaonesha ni namna gani Serikali zote mbili ya Muungano na ile ya Zanzibar zinavyoshirikiana kwa dhati.
Jamani jamani viongozi wetu tuoneeni huruma sisi wananchi wenu ambao hata uwezo wa kununua panadol hatuna achilia mbali milo mitatu kwa siku!!!!