Mwanaoshimba
Member
- Mar 8, 2017
- 61
- 82
Tumekuwa tukisikia mara kadhaa viongozi wa serikali, hasa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakitoa amri za ama kupiga marufuku uuzaji wa mahindi mabichi, uuzaji wa mahindi nje ya mikoa au wilaya zao, kutumia mahindi au mtama kwa ajili ya kutengeneza pombe au kutumia nafaka kwa ajili ya sherehe za kimila. Kinachonitatiza ni kuwa hivi, amri hizi zina uhalali gani? Na ni za haki?
Maana mkulima anahangaika kulima kwa gharama zake mwenyewe hadi anavuna pasipo msaada wa serikali. Sasa kwa nini serikali impangie namna ya kutumia mazao yake?
Kama hiyo inafanywa kwa manufaa ya wananchi, kwa nini pia kusiwe na amri za kufanana na hizo kwa wafanyakazi na wafanyabiashara? Mfano marufuku kutumia mshahara kwa ajili ya pombe au kugharimia mchepuko, au pengine marufuku sherehe za harusi kutumia gharama zinazozidi mil 2.
Maana amri zinapotolewa upande mmoja tu inakuwa ni double standard. Inaonekana kama vile mkulima ni kibarua wa wafanyakazi na wafanyabiashara. Hana maamuzi juu ya mazao yake. Upande wa wasiolima ukiona kuna hatari ya njaa na kupanda bei ya chakula wanampangia afanye nini ili wasije kuathirika na kupata tabu.