Jef Kirhiku
Member
- Dec 10, 2016
- 39
- 76
Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa yenye ng'ombe wengi hapa nchini .
Kwa hiyo yanapatikana ,maziwa ,nyama na hata ngozi kutokana na wanyama hao .
Wako wafugaji wanaojaribu kuyaongeza thamani maziwa ya Ng'ombe kabla ya kuyauza kwa kuyagandisha na kuyafungasha kisha kuyauza Kwenye maeneo yao .
Wanafungasha kwa kiwango kidogo kufikia lita 10,20, hadi 30 za maziwa kwa siku .
Na maandalizi ya maziwa haya wanayafanyia nyumbani kutokana na mitaji midogo ya kuanzisha viwanda .
Kwa bahati mbaya viongozi na mamlaka mbalimbali mkoani Singida, wameamua kuwafungia hawa wajasiriamali wadogo wanaothubutu kuzalisha bidhaa wasifanye hivyo kwa kile wanachokidai hawana vibali .
Badala ya kuwasaidia kukuza mitaji yao ili hatimaye waweze kukuza shughuli zao wanawafungia .
Tafsiri yake ni kwamba hawa kina mama wabaki kuwa wachuuzi wa bidhaa zinazozalishwa na wakubwa .
Waendelee kuuza maziwa ya wakubwa kwa kuwa tuu wao hawawezi kumudu masharti magumu yaliyowekwa ili kuruhusiwa kufanya shughuli hizo .
Hiyo Tanzania ya viwanda itashuka kama mvua bila kuwawezesha hawa wadogo wanaothubutu kuongeza thamani ya mazao yanayopatikana maeneo yao ?
Viongozi wa mkoa na wilaya Singida mnao wajibu wa kuwasaidia hawa wajasiriamali wadogo sio kupanga njama za kuwafungia .Mnapaswa kumsaidia Rais kuunga mkono juhudi za kuongeza thamani ya mazao zinazofanywa Kwenye maeneo yenu badala ya kukwamisha kwa maslahi ya wazalishaji wakubwa.
Juhudi za wajasiriamali wadogo kuonana na Rais kumweleza kero zao zinaendelea .