Viongozi wa mji wa nzega hii aibu

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,611
9,814
Katika ulimwengu wa sasa ambao teknolojia ya habari na mawasiliano mji kama wa nzega wa zamani kukosa kituo cha radio ambacho kinasikika ndani ya mji wa nzega tu jamani hii aibu

Huu mji asilimia ya wakazi wake ni watu wa mashambani ambao wengi wao wanatumia lugha ya asili kisukuma au kinyamwezi sasa hawa watu pasipo kupata habari mbali mbali kuhusu afya, uchumi, elimu, siasa nk si ndio wanazidi kubaki nyuma kwani radio ambazo zinasikika mjini nzega kama clouds, radio free afrika na kiss fm zinatumia lugha ya kiswahili na hizi radio Kuna maeneo hazisikiki kabisa ukienda uko ni mwendo wa mziki tu waioifazi kwenye memori kadi

Wito wangu kwa wakazi wa nzega na wadau wa masuala ya TEHAMA mliopo nzega ebu amkeni fungueni kituo cha radio mfungue fulsa zilizojifisha

Mfano biashara leo hii ukifika nzega ukiwa na tukio au mkutano ukitaka uitishe watu ni ngumu maana hakuna chombo cha haraka haraka cha habari cha kuamasisha watu waje

Miye na imani kituo kikifunguliwa mjini nzega watapata matangazo mengi tu hususani makampuni ya sm pembe jeo nk cha muhimu vipindi na maudhui ya hiyo radio yaendane na wakazi wengi wa nzega ambao wapo vijijini uko

Bye bye nzega
 
Na wakazi wa Kaliua nao watasema hivyo hivyo, omba vituo vilivyopo viimarishe na kuboresha Huduma zake ili ziwafikie watu wote Tanzania ikiwepo nzega
 
Back
Top Bottom