Viongozi wa kiroho na chaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa kiroho na chaguzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mch Kasimbazi, Apr 2, 2012.

 1. M

  Mch Kasimbazi Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi niliye mdogo miongoni mwao wote naomba kuleta wazo hili. Katika zama hizi za siasa za vyama vingi ni vizuri tuwe waagalifu na hila na ujanja wa kugawa sharika na waumini wetu kupitia migawanyiko ya kisiasa. Ni vyema kutokubali kwa mfano wakati wa kampeni kuingia kichwa kichwa katika ushabiki wa wagombea bila kuomba na kupata uongozi wa Mungu. Inapotokea ukasimama mbele ya waumini na kuwaambia mchangue fulani maana Mungu amemkubali, halafu watu hao hao waone huyo mtu kesho akishindwa uchanguzi; au akashinda uchaguzi lakini akawa mwiba kwa maendeleo ya watu, lawama zote wanazirudisha kwa viongozi wao wa kiroho. Viongozi wa kiroho wanapaswa kusimama kinabii na kuleta moyo na mawazo ya Mungu kwa watu.

  Ikiwa ni kweli taarifa zilizoenea katika magazeti ya Mwanahalsi kuwa wachungaji na maaskofu walikuwa wananunuliwa huko Arumeru ili wakisaidia chama cha mapinduzi nafikiri hilo si sawa. Si kwamba si sawa kusimama na CCM, la bali si sawa kuvutwa na pesa badala ya kuongozwa na Mungu. Ni vizuri watumishi wa Mungu tuombe na kusimama upande wa Mungu na tusiwalazimishe washirika kufuata matakwa yetu ya kisiasa. Huko nyuma wanasiasa wamejaribu kututumia na baada ya hapo hawakujali hata maslahi yetu (kama kanisa) badala yake wamekuwa wakitutupia lawama kila kukicha kuwa sisi ni chanzo cha siasa mbovu za udini. Tutunze heshima ya Mungu tunayemtumikia.

  Nawasilisha.
   
 2. A

  ATA Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  You have said it all, na msiwe waoga kukemea uovu unaofanywa na watawala wetu, simamieni haki bila upendeleo na wala msiogope na vitisho vya watawala waovu.
   
Loading...