Viongozi wa dini waonya, wataka muafaka haraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini waonya, wataka muafaka haraka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 13, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,733
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Serikali, Chadema bado hapatoshi
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 12 November 2011 21:06
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  VIONGOZI WA DINI WAONYA, WATAKATA MUAFAKA HARAKA
  Na Waandishi wetu
  Mwananchi

  MSUGUANO kati ya Serikali na Chadema sasa ni bayana kufuatia kauli mbalimbali za viongozi wa Serikali kukosoa hadharani mwenendo na utendaji wa chama hicho kikuu cha upinzania nchini.

  Hatua hii imekuja wakati hali tete ya kisiasa ikiendelea kugubika Jiji la Arusha huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiri hadharani kuwa maandamano yanayofanywa na Chadema kwa kaulimbiu ya 'Nguvu ya umma,' yanainyima usingizi serikali.

  Mbali na Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulungo, amekuja juu na kudai kuwa harakati zinazoendeshwa sasa na Chadema, hazina nia njema na kwamba ni mkakati wa maksudi kutaka mkoa huo usitawalike.

  Wachunguzi wa mambo ya siasa nchini wanatafsiri kauli za viongozi hao kuwa zimefungua ukurasa mpya unaodhihirisha kuwepo msuguano mkubwa na wazi kati ya Serikali na Chadema.

  Kwa muda mrefu Chadema imekuwa ikilaumu mambo kadhaa ikiwemo kunyimwa vibali vya maandamano na makada wake kuswekwa rumande na kudai kwamba nyuma ya matukio hayo, kuna mkono wa Serikali.

  Mwanzoni mwa wiki hii viongozi wa Chadema akiwamo, Katibu Mkuu wake, Dk Wilbroad Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu walikamatwa kwa kosa la kufanya mkusanyiko bila kibali cha polisi katika Uwanja wa NMC mjini Arusha.

  Hata hivyo, hatua hiyo inaonekana kupingwa na baadhi ya viongozi wa dini, wanasiasa na wafanyabiashara mkoani Arusha kwa maelezo kwamba vurugu, vitisho na matumizi ya vyombo vya dola kamwe hayawezi kuleta suluhu ya migogoro ya kisiasa na kushauri kuwepo mazungumzo na majadiliano kati ya makundi husika.

  Kauli za viongozi wa dini
  Wakizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti jana, Askofu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer na Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Wilaya ya Arusha, Abbas Ramadhani Mkindi ‘Darweshi,' kwa pamoja waliwataka viongozi wa serikali na vyama vya siasa mkoani Arusha, kuacha ubabe, vitisho na kuhasimiana badala yake waonyeshe nia ya kweli kumaliza mgogoro huo.

  "Hali ni mbaya Arusha katika nyanja zote. Kisiasa kuna machafuko yanayotuathiri wote, waliomo na tusiokuwemo. Katika matatizo na machafuko haya, huwezi kunyooshea kidole mtu au chama chochote cha siasa, muhimu hivi sasa ni kufanyika majadiliano bila ubaguzi wala kudharauliana ili turejeshe amani mjini mwetu," alishauri Askofu Laizer alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.

  Askofu huyo, alisema Arusha inahitaji viongozi makini wanaozingatia utawala wa sheria, diplomasia na wenye staha katika kushughulikia changamoto zilizopo, kama mgawanyiko mkubwa wa kiitikadi ulioibuka kati ya wafuasi wa CCM na Chadema.

  Kongozi huyo wa kidini mwenye ushawishi na msimamo usioyumba katika mambo yanayohusu jamii, alisema vitisho vya watawala na matumizi ya vyombo vya dola haviwezi kutatua tatizo la Arusha, bali vinaweza kupooza kwa muda na baadaye mambo hayo yataibuka kwa nguvu na mbinu mpya na kusababisha vurugu zaidi.

  Alionya kuwa si busara kupuuza madai ya Chadema na kuwashauri viongozi wa Serikali kuacha kutumia nguvu yadola kutunishiana misuli na chama hicho kwani Arusha inaelekea pabaya na likitokea la kutokea, wote watangamia.

  ''Lazima busara itumike kwa kusikiliza hoja za pande zote husika bila kubezana.'' Alishauri.


  Bila kutaja jina, Askofu Laizer alisema kauli za vitisho zinazotolewa na viongozi wa serikali Arusha, zitachochea harakati za wanaodhani wanaonewa, kutafuta haki na pengine kutumia njia za machafuko zaidi na kuchafua hali ya hewa kuliko livyo sasa.

  Askofu Lazier alivishauri vyama vya upinzani kuepusha shari kwa kudai haki zao kwa njia ya amani hata kama wanahisi kuonewa, kama ilivyo kwa Arusha ambapo vijana wa CCM (UVCCM), waliandamana na kufanya mkutano wa hadhara bila kibali cha polisi, lakini Chadema walipojaribu kufanya hivyo, walikamatwa na kushtakiwa
  kwa kusanyiko lisilo halali.

  "Vyama vya upinzani vikwepe pale sunami au upepo mkali unapovuma dhidi yao, wainame kidogo kimbunga kipite halafu waendelee mbele.

  "Vitumie wataalamu na wasomi waliojaa ndani ya vyama hivyo kutatua matatizo na migogoro inayojitokeza kwa njia ya amani na utulivu," aliasa Askofu Laizer.

  Alisema tatizo linalojitokeza nchini hivi sasa ni vyama vya upinzani kutopewa fursa ya kutekeleza na kuendesha shughuli zao za kisiasa kwa uhuru kama ilivyo kwa CCM.
  Hata hivyo, alivashauri vyama hivyo kufuata sheria na kanuni katika kudai na kutafuta haki yao .

  Kwa upande wake, Mkindi alisema viongozi serikalini wasijidanganye kuwa wanaweza kulinda amani kwa mtutu wa bunduki na kushauri vyama vinavyohasimiana vya CCM na Chadema kukutanishwa ili vijadili na kuondoa tofauti zao ili kurejesha amani na usalama Arusha.

  "Arusha imechafuka, hakuna amani. Biashara imekufa, hata mikutano ya kitaifa na kimataifa haifanyiki hapa tena kwa wingi kama ilivyozoeleka. Ufumbuzi ni watu kukaa mezani wazungumze, waadiliane na kutatua tofauti zao.

  ''Chadema wasidharauliwe hata kidogo kwa sababu wana watu wengi wanaowaunga mkono ambao wako tayari kusikiliza na kutekeleza lolote wanaloambiwa," alisema Mkindi

  Msimamo wa RC Arusha

  Katika siku za karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mulongo amekaririwa akionya kuwa vyombo vya dola vimejipanga kukabiliana na aliowaita, wavuruga amani na waleta machafuko Arusha, na kuelekeza
  mashambulizi ya moja kwa moja kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na chama chake.

  "Nikiwa mhimili na msimamizi wa amani na usalama wa mkoa, sitakubali kushuhudia mtu anavuruga amani tena Arusha. Kibaya zaidi wengi wa wanaoleta vurugu hapa wanatoka nje ya mkoa wetu. Imetosha! Tumechoka," alikaririwa mkuu huyo wa mkoa alipozungumza na viongozi na watendaji wa manispaa ya jiji hilo.

  Mgogoro wa Arusha
  Tangu kumalizika uchaguzi mkuu mwaka jana na ule wa umeya, mji wa Arusha umekumbwa na mfululizo wa machafuko yanayoambatana na matumizi ya nguvu ya dola kuyakabili.

  Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, wanachama na wanachama wengine wa Chadema hadi sasa wameendelea kujikuta wahanga wa hali hiyo kwa kuswekwa ndani na kufunguliwa kesi mahakamani.

  Hadi kufikia Alhamisi wiki hii, viongozi wakuu wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Slaa, wanasiasa na wanachama kadhaa wa chama hicho, nao wamejikuta wakikabiliwa na kesi sita tofauti kwa kudaiwa kushiriki mkusanyiko usio halali na kukaidi amri halali ya polisi.

  Mwafaka CCM na Chadema
  Kwa upande wao, viongozi wa Chadema na CCM waliunga mkono hoja ya kujadilina ili kutafuta muafaka wa mgogoro wa Arusha kwa njia ya majadiliano, huku kila upande ukisisitiza kuaminiana na kuheshimiana huku Chadema wakiwatuhumu viongozi wa serikali mkoani Arusha kuwahukumu bila kuwasikiliza malalamiko na hoja zao.

  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Mkoa wa Arusha, Ephatah Nanyaro, alisema alisema chama chake kiko tayari kujadiliana na yeyote kuhusu amani na mustakabali wa Arusha na kusisitiza kuwa lazima watawala watambue kuwa hawapigi kelele kwa lengo la kufanya mkoa usitawalike kama inavyodaiwa.

  Kwa upande wake, Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Arusha, Semmy Kiondo alisema chama chake kiko tayari wakati wowote kukutana na kujadiliana na mtu, chama au chombo chochote ikiwemo Chadema kutafuta amani na maendeleo ya Arusha lakini akasisitiza hakiko tayari kutishiwa, kunikizwa wala kubezwa kwa namna yoyote.

  Bastola ya Slaa
  Katika hatua nyingine, Jeshi la polisi mkoani Arusha limetamka ya kwamba uchunguzi wa silaha mbili za moto walizokamatwa nazo,Dk Slaa pamoja na mfuasi wa chama hicho,Daniel Ongong'o Novemba 8 mwaka huu jijini Arusha bado haujakamilika. (Na uchunguzi kuhusu bastola ya Aden Rage umeshakamilika!?)

  Akihojiwa juu ya hatma ya uchunguzi wa silaha hizo jana Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo, Akili Mpwapwa alisema kuwa upepelezi juu ya uhalali wa umilikaji wa silaha hizo bado haujamilika kwa kuwa uchunguzi huo sio suala la muda mfupi.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Majibu kama haya yanadhalilisha na kuondoa uhalali wa kuwa na authorities. Ina maana Jeshi la polisi halina database ya silaha zinazomilikiwa na raia pamoja na majina ya wamiliki?, ninapata shaka hata kwenye suala la hati za nyumba, magari etc hakuna database.

  Dr Slaa si mwendawazimu kutembea na bastola ambayo si halali katika sehemu ambayo ana uhakika 100% Polisi watavamia na kumkamata, Mwema na surbodinate wako kama mnaona mnashindwa kufanya kazi kitaalam kwa kuingiliwa na wanasiasa si muachie ngazi tu?, huu ni udhalilishaji wa utendaji wenu si udhalilishaji wa Dr Slaa.

  Yaani unamkamata mtu na bastola yenye namba na hati za kuimiliki badala ya kuihakiki na kumrudishia tena bila kutangaza maana kama ana miliki kihalali unamtangazia nani?, hii spin sasa inakuwa too much. Na ninawahakikishia polisi kuwa kinachowafanya muendelee kuwa legitimate kwa mtazamo wenu ni kumilikiwenu wa maghala ya silaha basi ila wananchi hawana imani tena na polisi wa Tanzania, ndiyo maana watu wanajichukulia sheria mikononi tu.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,733
  Trophy Points: 280
  Vyombo vya dola kwa kutumiwa na Serikali taahira ya Magamba vinamtafuta Dr Slaa kwa kila hali ili vimfunge. Kama utakumbuka miaka michache iliyopita kulikutwa vinasa sauti chumbani kwa Dr Slaa wakati alipokuwa anahudhuria kikao cha Bunge kule Dodoma. Vyombo vya dola vikadai vinafanya uchunguzi lakini hadi hii leo hawajatangaza chochote kuhusu uchunguzi wao ulikofikia. Nchi yetu sasa imeoza, hili siyo siri vyombo vya dola vimekubali kutumiwa na magamba ili kupindisha sheria na kuwanyanyasa Watanzania wakiwemo Viongozi wa vyama vya upinzani hasa wa CHADEMA, lakini kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.
   
Loading...