Viongozi wa dini na matukio ya kuombewa, hakuna siasa ndani ya suala hili?..

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Juzi kwenye vyombo vya habari wameonekana viongozi wa madhehebu ya kikristo wakizungumzia suala la kumuomba Mungu ili mvua zinyeshe baada ya kipindi cha takriban mwezi mmoja wa joto kali.

Kipindi kile cha kuelekea uchaguzi, viongozi wa dini wakasikika sana wakiongelea suala la kuiombea nchi ipite kwa amani katika kipindi cha uchaguzi, ikabuniwa mpaka kauli isemayo "kuna maisha baada ya uchaguzi".

Huwa ninajiuliza ni sababu zipi ambazo huchangia katika kuibua hoja za viongozi wa dini kuhamasisha jamii juu ya kuliombea taifa katika kipindi fulani.

Ina maana kama mvua zingekuwa zinanyesha kwa wastani, tusingewaona viongozi hawa wa dini wakituhamasisha kumuomba Mungu atujalie mvua?.

Kuna ukahaba wa kutisha mitaani, kuna wale wanaoitwa watoto wa mitaani, wanaodhalilika kila siku pembeni ya barabara kubwa na kwenye korido za majengo. Ina maana yote haya sio sehemu ya majanga ya taifa hili?.

Naheshimu sana umuhimu wa viongozi wa dini, lakini ninajiuliza maswali mengi kuhusiana na umuhimu wa suala linalofaa kuombewa katika kipindi fulani. Nadhani kwamba mambo yenye kufaa kusisitiziwa ili yaombewe na wanajamii ni wengi. Ni bora yakawa yanapewa umuhimu wa mara kwa mara na sio viongozi wa kidini waishie kuonekana wakati wa kipindi cha kuelekea uchaguzi na wakati nchi yetu ikikumbwa na ukame usiotarajiwa.
 
Back
Top Bottom