kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,931
- 7,828
Viongozi wa chadema sasa wanakibomoa chama kwa mikono yao wenyewe kutokana na ubinafsi na kiburi. Huko nyuma tumeona waanzilishi wa vyama vya siasa nchini wakiviona vyama hivyo kama kampuni zao binafsi tukadhani chadema ni tofauti. Tatizo kubwa la zzk katika chadema ni pale alipoonyesha nia ya kutaka kukiongoza chama chake jambo ambalo ni haki ya kikatiba ya kila mwanachama. Kwa maoni yangu naona wapo watu wanaona wana hisa kwenye cdm na wao tu ndio wanaoweza kuongoza au kuamua nani awe kiongozi wa chama hicho. Tatizo la kuwafukuza vijana ovyo ovyo badala ya kuwalea au kuwaadabisha kwa njia ya kufaa ni mbaya. Wao wanajiamini na wanaona wanaweza kwa hivyo n wajibu wa watu wazima katika chama kuwaelimisha kwani katika uongozi hekima na busara sifa zinazopatikana zaidi kwa watu wazima ni muhimu sana. cdm lazima itambue kwamba ni tegemeo kubwa hata kwa wanaccm wanaojali maslahi ya taifa kwa hivyo ni muhimu wao kusuluhisha tofauti zao kwa busara.