Viongozi wa Afrika

Viongozi wa Afrika

8691jakigili

Senior Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
178
Reaction score
67
Viongozi wa jana wa Afrika ni sawa tu na wa leo. Ni wachache sana viongozi wa Afrika ambao hawaangukii katika mkondo huu. Ninaamini Afrika haiwezi kuendelea iwapo viongozi ni wale wale - wa jana ni sawa na wa leo. Kwa mfano, hapa Tanzania tumefanikiwa kuwa na viongozi awamu nne sasa, ukimwondoa baba wa taifa, Nyerere. Hawa waliofuata wana tabia na mitazamo inayofanana kwa karibu sana. Nisaidie kujua sababu ni zipi hasa viongozi wetu wa jana kufanana na wa leo? Daniel Arap Moi ni sawa na Kibaki kwa mambo mengi, na Kibaki ni sawa na ajaye!!! Nchi zetu za Afrika zimebakia na matatizo yaleyale: umaskini, ujinga na maradhi!! Kwa nini?
 
Tukipata viongozi wenye mitazamo tofauti wanapigwa majungu na tabaka tawala kwamba wanatafuta umaarufu..mwakyembe..sokoine..mrema..magufuri nk,watu wazuri wenye mawazo mapya wapo lakini mfumo unawabadilisha
 
Kwa nini viongozi wapya wanaogopa kubadilisha mifumo iliyotangulia isiyo na tija? Kwa mfano, viongozi wa Bara la Asia ambao nao walitawaliwa na wakoloni na kudai uhuru kipindi karibu sawa na nchi za Afrika, wamebadilisha mifumo na wako mbali kimaendeleo.
 
Kwa nini viongozi wapya wanaogopa kubadilisha mifumo iliyotangulia isiyo na tija? Kwa mfano, viongozi wa Bara la Asia ambao nao walitawaliwa na wakoloni na kudai uhuru kipindi karibu sawa na nchi za Afrika, wamebadilisha mifumo na wako mbali kimaendeleo.
hakuna uthubutu mkuu,hembu fikiri Mama Sijaona alikua katibu mkuu ardhi akapima viwanja 20000.akataka kugombea ubunge tabora kwa mheshimiwa kapuya au sitta,akalazimishwa aache na kupelekwa japan mafichoni.na miradi ardhi imekufa
 
Back
Top Bottom