Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,439
- 6,691
Sema kuna muda hawa ACT wanapenda sana drama.
Hivi kweli unaaanda press then unaanza kuwaambia waandishi kwamba CCM ianze kujishughulikia wenyewe? Hawa wataweza kweli zile "siasa za mapambano" ambazo huyo Othman alikuwa anazizungumzia?
=============================================
Chama cha ACT Wazalendo kimeiomba Serikali kuwachukulia hatua viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti Bara, Stephen Wasira, na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa CCM-Zanzibar, Hamis Mbeto, kwa kupotosha umma kuhusu tukio lililotokea nchini Angola.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Wito huo umetolewa leo, Jumapili, Machi 16, 2025, na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Taifa, alipozungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Magomeni, jijini Dar es Salaam.
“Niseme wito wangu kwamba hasa kwa haya ambayo yamepotoshwa na watu ambao ni waandamizi wa Chama cha Mapinduzi, naiomba sana Serikali na natoa wito serikalini kama Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo kwamba Serikali iwachukulie hatua viongozi hao, kwa sababu upotoshaji wao umeipaka matope Serikali. Upotoshaji wao umewafadhaisha wananchi kwa kiasi kikubwa, wamefanya vitu kwa namna ambayo haiendani na nafasi zao, huo ndiyo wito wetu kama ACT,” amesema Othman.
Machi 14, akizungumza Tunduma mkoani Songwe, Wassira alisema: "Leo nimesoma viongozi walikuwa wanaenda Angola lakini wamenyang'anywa paspoti huko ni Angola sio hapa, hapa hatuja wanyang'anya paspoti na hata ikimaliza muda wake tunawapa, ili waende wanakotaka alafu warudi salama.
“Wamelalamika kwa nini Serikali imekaa kimya kwani sisi tunasimamia Airpoti ya Angola? Airpoti ya Angola inasimamiwa na watu wa Angola, na pia huenda walikuwa na jambo lao ambalo wanalilitilia shaka wangeuawa tungesema kwa nini wamewaonea watu wasiokuwa na hatia," amesema Wassira.
Viongozi wa ACT Wazalendo walizuiwa kuingia nchini Angola kushiriki katika mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD), yaliandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation.
Source: Mwananchi