Viongozi mnaohama vyama kuunga mkono juhudi za kiongozi fulani ni Ushamba,Jifunzeni kwa John Shibuda

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
John Shibuda alikua ni Mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki kupitia CHADEMA awamu ya tano.Mwanasiasa huyu aliunga mkono juhudi za serikali ya CCM wakati huo mwanzo hadi mwisho wa ubunge wake, hatukuwahi kusikia eti anajiuzulu ubunge ili akaendelee kuiunga mkono serikali, na wala CHADEMA hawakuwahi kumufukuza tu kwa sababu alikua anaiunga mikono serikali ya CCM. Hawa wanasiasa wetu wa sasa wana matatizo gani? Ni ushamba wa kisiasa?

Inashangaza kuona kiongozi mzima tena msomi mzuri kabisa anaamua kuwaacha wananchi waliomwamini anahama chama kwa sababu tu anamuunga mkono kiongozi flani, huu ni ushamba na usaliti wa wananchi unaosukumwa na maslahi binafsi ingawa ni haki yake kikatiba kufanya hivyo. Kizuri ni kwamba zile video za Mh Nassari zilijieleza wazi kua wananunuliwa kwahiyo wasihadae wananchi kua wanahama kuunga mkono juhudi za kiongozi flani, huu ni uongo!

Nimemtaja Mh Shibuda kama sample tu lakini kulikua na wabunge kama Mrema, Cheyo na wengineo ambao siku zao zote za ubunge ilikua ni dhahiri kua wanaiunga mkono serikali ya CCM na hawakuwahi kuhama vyama vyao wala kufukuzwa. Hii awamu tunashudia mambo ya ajabu kabisa tukifikiri kufanya hivyo ni kulisaidia taifa kumbe tunaliangamiza.

Viongozi wa aina hii hawana huruma, hawajali walalahoi wanaoteseka kukosa utetezi wao, naweza kusema kua roho zao zimetawaliwa na umimi. Wameamua kuweka elimu zao mifukoni na kuamua kuendeshwa na matamanio ya dunia.Hawa sio wanasiasa ispokua jina sahihi lingependeza zaidi wakiitwa wasanii wa kisiasa na hata siku moja hawatokaa waaminike tena maishani mwao. Maamuzi na hoja zinazowapelekea kuhama hayaingii akilini kwa wenye kufikiria sawa sawa.
 
Na hata huko wanakohamia hamna lolote ni ubinafsi wao tu unawapeleka hawana uzalendo wowote katika utendaji wao wanasaka maisha yao tu hawa ndio ambao hata kule walikohama na kwenda kwingine wakipewa hata ukuu wa wilaya hawatafanya lolote zaidi ya tumbo lake nonsense.
 
Na hata huko wanakohamia hamna lolote ni ubinafsi wao tu unawapeleka hawana uzalendo wowote katika utendaji wao wanasaka maisha yao tu hawa ndio ambao hata kule walikohama na kwenda kwingine wakipewa hata ukuu wa wilaya hawatafanya lolote zaidi ya tumbo lake nonsense.
Mtu kama Dr Moleli anadai eti ameona mbali, khaa ameona mbali kitu gani zaidi ya ubunge? Ameona mbali kwenye tumbo lake?
 
Back
Top Bottom