Viongozi Mnaipeleka nchi Kubaya

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
[MODS TAFADHALI MSIFUTE HII MADA] !

Kinachoendelea nchini Tanzania ni chimbuko la machafuko makubwa isipodhibitiwa. Haya yalitokea Libya, Tunisia na Misri. Nina maana ya kwamba kuna ubaguzi mkubwa kuanzia kwenye elimu hadi kwenye haki zetu za msingi kaka ajira. Viongozi wetu wamekuwa wakichochea machafuko kwa kutumia dhamana tuliyowapa vibaya kutunyima haki zetu za msingi.

  • Nafasi za masomo zinapotoka nje ya nchi, hawa wakubwa wanakusanya watoto wao kwa njia za panya na kuwapeleka kusoma katika vyuo vyenye hadhi kubwa
  • Nafasi za kazi, kwenye ubalozi, mashirika ya umma kama TRA, NSSF, BoT nk… ni watoto wao ndio wanaongizwa bila kuzingatia “qualifications” mbaya zaidi hawa vijana wana arrogance mbaya sana na dharau kwetu sisi watoto wa masikini. Mfano ni wale wanaofanya kazi kwenye mabalozi na BOT
  • Kwenye siasa wanalazimisha na hata kufikia kupindisha taratibu ili kuwapa watoto wao madaraka.
  • Watoto wa wakubwa wanafanya uonevu mkubwa mtaani, lakini ukipeleka uonevu wao kwenye vyombo vya dola na mahakama, unageuziwa wewe kesiWatoto wao wamekuwa kama viongozi, wanajilimbikizia mali, wanafanya ufisadi kila idara ya serikali. Wanadiriki kuwatishia maisha yeyote anayepinga matakwa yao
Kinachoendelea itafika muda haitavumilika, wote walioingizwa kwenye nafasi kubwa kutokana na nafasi za wazazi wao watapata wakati mgumu siku za mbeleni,
 
Uliyoandika ni mambo ya busara na kweli ndiyo yanayotendeka nchi hii, tunaona hata kwenye siasa viongozi wanataka kuwarithisha watoto wao utawala!! Itabidi pachimbike nchi hii siku za usoni kwani watoto wa maskini uzalendo karibu unawashinda.
 
[MODS TAFADHALI MSIFUTE HII MADA] !

Kinachoendelea nchini Tanzania ni chimbuko la machafuko makubwa isipodhibitiwa. Haya yalitokea Libya, Tunisia na Misri. Nina maana ya kwamba kuna ubaguzi mkubwa kuanzia kwenye elimu hadi kwenye haki zetu za msingi kaka ajira. Viongozi wetu wamekuwa wakichochea machafuko kwa kutumia dhamana tuliyowapa vibaya kutunyima haki zetu za msingi.

  • Nafasi za masomo zinapotoka nje ya nchi, hawa wakubwa wanakusanya watoto wao kwa njia za panya na kuwapeleka kusoma katika vyuo vyenye hadhi kubwa
  • Nafasi za kazi, kwenye ubalozi, mashirika ya umma kama TRA, NSSF, BoT nk… ni watoto wao ndio wanaongizwa bila kuzingatia "qualifications" mbaya zaidi hawa vijana wana arrogance mbaya sana na dharau kwetu sisi watoto wa masikini. Mfano ni wale wanaofanya kazi kwenye mabalozi na BOT
  • Kwenye siasa wanalazimisha na hata kufikia kupindisha taratibu ili kuwapa watoto wao madaraka.
  • Watoto wa wakubwa wanafanya uonevu mkubwa mtaani, lakini ukipeleka uonevu wao kwenye vyombo vya dola na mahakama, unageuziwa wewe kesiWatoto wao wamekuwa kama viongozi, wanajilimbikizia mali, wanafanya ufisadi kila idara ya serikali. Wanadiriki kuwatishia maisha yeyote anayepinga matakwa yao
Kinachoendelea itafika muda haitavumilika, wote walioingizwa kwenye nafasi kubwa kutokana na nafasi za wazazi wao watapata wakati mgumu siku za mbeleni,

kama wewe ni mke wa muzungu kalalamike kunako husika
 
jibu rahisi tuu .piga chini hii chama cha mafisadi anza kampeni sasa ,2015 tunaagana na hayo yote uliyo lalamika .
 
Miaka50 ya uhuru tunajivunia amani na utulivu, TUMETHUBUTU TUMEWEZA, na TUNASONGA MBELE...... Hivyo ndivyo tunavyoaminishwa..haya bana. Back to topic, ukitafakari kwa makini ule usemi ''Madaraka hulevya lakini pia hupofusha'' utakubaliana nami kuwa watawala wetu wamefika mahali wanafanya mambo hovyo hovyo (kilevi levi) na mbaya zaidi stimu zimekuwa za kudumu kwamba kila siku wao wamelewa.......... Wamepofuka kiasi kwamba hawaoni na si kwamba hawataki kuona ila mvinyo umepofusha kuanzia macho mpaka ufahamu...na ndio maana kwao kuwarisisha wanao nafasi za uongozi sio kitu na pia ajira zenye hadhi.. Sababu nlikwisha itoa hapo juu, lakini kubwa zaidi baadhi yao sio wacha Mungu na ndio maana adha zote hizi zinatukumba. Nawasilisha
 
waacheni watoto wa wakubwa wale raha.................hii yote ni matokeo ya maamuzi yetu.
 
2015 tunaagana na hayo yote uliyo lalamika
song3.jpg
song2.jpg

song4.jpg
 
Mbona unatoa lawama zisizo na kichwa wala miguu.
Fanya kazi acha kulalala
OTIS
 
Walishaipeleka nchi mortuary, wanachofanya sasahv ni kuchonga jeneza.
 
pole ndugu hivi ndiyo umelijua hilo leo. Tanzania baada ya Nyerere ikaugua ugonjwa huo wa Technical know who...., wanaokwenda India kutibiwa mwendo huo huo, ukitafuta kazi mwendo huo huo, shule nzuri mwendo huo huo, scholarships mwendo huo huo wa technical know who, kulindana makosa ni mwendo huo huo, uwekezaji kwenye maeneo nyeti mwendo huo huo. Siku tukitambua na kupractice technical know how, basi hatua ya kuleta maendeleo na mabadiliko ndiyo itaanza kuzaliwa. Na hiyo ni hatua moja nzuri sana
 
Back
Top Bottom