Poleni sana kwa majukumu ya kujenga taifa. Hivi naomba kuwauliza viongozi wangu wa ubungo ni barabara ngapi zipo kwenye bajeti ya kujengwa kwa mwaka ujao wa fedha na ni zipi? Naomba nitajiwe na zile mtakazozijenga kwa kiwango cha lami na ambazo mtaweka japo vifusi. Naongea hayo yote kwa maana kati ya wilaya ambayo ina barabara mbovu kwa Dar ni Ubungo. Maeneo yote ya mpigi magoe hayatamaniki, barabara hazipitiki kabisa. Nimeenda barabara moja inatokea machimbo kuelekea anapoishi mkuu wa wilaya kisarawe lakini haitamaniki hiyo bararaba. Lakini ukifuatilia ni barabara kubwa inayostahili japo kuwekwa kifusi.