Viongozi hawa wanaisumbua CHADEMA Singida

Viongozi hawa wanaisumbua CHADEMA Singida

chadema tunakoelekea siko,viongozi wa ngazi za juu wameweka pamba masikioni kila mtu ndani ya chama sasa ni kama kambale.

Ziumiazo ni nyika na ni neema sana kwa CCM piganeni wenyewe tuwakute mpo hoi tuwapige kama paka mwizi 2015......hiki chama yaani migogoro kila ck na sembuse Singida hamna chenu basi Isango endelea kutuneemesha na kazi tuliokutuma inafanyika vyema.....good job! WAJIFYA SANA
 
Basi utasikia magamba at work yaani.....kugombana munagombana wenyewe munalaumu CCM hata ugomvi wenu wa kugombea madaraka...tutayasikia mengi sana sembuse uchaguzi upo njiani mtatwangana sana mwaka huu na ndio utakuwa mwisho wenu.
 
Pamoja na changamoto kubwa za kimazingira zinazotukabili katika kuijenga CHADEMA mkoa wa Singida, wamekuwapo baadhi ya viongozi ambao wamekuwa mzigo mzito na kwa namna moja au nyingine wanatukwamisha.

Hao ni pamoja na aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la singida mjini, Josephat Isango na anayekaimu nafasi ya Katibu wa BAVICHA kwa sasa, Timothy Peter Thomas. Viongozi hawa mara nyingi wamekuwa wakikataa kushirikiana na wengine , wakiwemo viongozi wa BAVICHA mkoa wakijidai kuendeleza sera ya usomi ndani ya CHADEMA. Mathalani, wote wawili wamekataa kushiriki mikutano iliyoandaliwa na chama mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu na ile iliyoandaliwa mapema na mjumbe wa kamati kuu, Dr. Kitila Kikumbo.

Pia, wamekuwa na uhasama kwa muda mrefu hadi kufikia hatua ya kutishiana maisha wao kwa wao, uhasama ambao wengi tunauhusisha na mbio za kuwania ubunge waka 2015 kwani wote wanaonekana wanautaka. Wote waliamua kukwamisha kwa makusudi kabisa mashindano ya BAVICHA wilaya ya Singida mjini mwishoni mwa mwaka jana, mashindano ambayo yaliandaliwa na mwenyekiti wa chama wilaya ya singida nddugu Kumalija.

Josephat Isango
, ambaye alivuliwa uenyekiti wa BAVICHA kutokana na kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 na baada ya kukmbwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za chama ameendelea kung'ang'ania uongozi na amekuwa akitoa matamko kwa niaba ya viongozi tulioko Singida akidanganya ameyatoa makao makuu ya chama.

Timothy Peter Thomas
naye, ambaye bado hajakomaa katika siasa za mikikimikiki anasemekana aliilazimisha kamati tendaji ya wilaya ili impe nafasi ya BAVICHA wakati mara nyingi yuko chuoni Dar es salaam na mwaka jana aligombana na Katibu wa wilaya, Yahaya Ramadhani baada ya kukaimu kwa nguvu nafasi ya katibu wa wilaya. Wote wawili pia wamekuwa wakitoa lugha mbaya kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoani hapa akiwemo Katibu wa wilaya, Yahaya Ramadhani. Ndugu Yahaya ameyathibitisha yote haya katika mazungumzo niliyofanya nae wiki iliyopita tukiwa ofisini, Singida.
CHANZO : MIMI MWENYEWE
Chanzo kwanza sio credible, halafu la pili, wewe huna sifa ya uongozi ndani ya CDM, kama kiongozi hili sio jambo la kuweka JF, ungeandika barua kwa mamlaka husika/ya juu kutoa malalamiko kuliko hiki ulichofanya. Nyie ndo tunawambia kila siku hamjabalee kisiasa. Mkishabalee mtaacha hoja hizi za kitoto za kushutumiana hadharani. Lazima uelewe pia uongozi uongozi mda mwingine ni kubeba hata unavyotamani kusema hadharani, lakini kwa kupima madhara yake kwa chama huwezi kusema kila kitu. Wewe unadhani unamdhailisha/umemsemelea Isango kumbe unadhalilisha CDM ambayo ina maskalai mapana kwa Watanzania wote kwamba haina viongozi makini wapo tu vihio kama wewe. Acha utoto wako wa kusema hovyo.
 
Yaani sikuwahi kujua kama CDM wanamzigo mzito hivi. Yaani wamekalia umbeyaumbeya kama wametumwa vile, hawa wangekuwa CCM tungesikia vifo vya presha kwa vijana vingi sana. Waache umbeya wajenge Chama huko

Huyo inawezekana hata si CHADEMA.........yuko kazini!
 
Back
Top Bottom