Viongozi hawa wanaisumbua CHADEMA Singida

Viongozi hawa wanaisumbua CHADEMA Singida

Kwanini mnagombania vyeo? Mbowe alisema chadema si kichaka cha wasaka vyeo, mmesahau?
 
Halafu Isango ni mlevi sana, muongo na mbabaishaji. Anajifanya mjuaji wa kila kitu akipata ef 10 tu mbio hadi bar
 
Wajisahihishe ili kulinda imani ya wananchi kwa CHADEMA.
 
wanakosea sana..

Nina wasiwasi kama wewe hujatumwa na Mchemba ili uvuruge chama kwani kama kweli tuhuma zako ni za kweli, kwanini usitumie taratibu za kawaida kuwasilisha malalamiko kwa chama kwa kuandika barua kwa katibu wa mkoa na nakala kwa katibu mkuu au kapeleka tuhuma zako kwenye mikutano halali ya chama.
Humu jf unamwaga mchele kwenye kuku wengi wengine ni kunguru.
Tumia akili sana ktk kujenga sio kubomoa.
 
wanakosea sana..

Kwanini mambo ya ndani ya Chama mnayaleta JF??? Hivi mnategemea hapa ndiko vinakopatikana vikao husika vya chama? I guess wewe ndio tatizo wa kwanza alafu wao ndio wanafuata. Mode hawa wanaojifanya kuleta mambo ya ndani ya vyama vyao kwa fake ID nashauri wawe wanapigwa ban unless aje na verified ID
 
Akili yangu inanituma niamini kwamba huyu anatengeneza mgogogro tu wa kipropaganda zaidi. Nafikiri lengo lake ni kuchafua hali ya hewa tu kwani ana uzi mwingine tena anamzungumzia Isango kwamba amekula 1M ya kusaidia wahanga wa vurugu za Ndago. Nahisi huu ni mkakati maalum tu.
 
Pamoja na changamoto kubwa za kimazingira zinazotukabili katika kuijenga CHADEMA mkoa wa Singida, wamekuwapo baadhi ya viongozi ambao wamekuwa mzigo mzito na kwa namna moja au nyingine wanatukwamisha. Hao ni pamoja na aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la singida mjini, Josephat Isango na anayekaimu nafasi ya Katibu wa BAVICHA kwa sasa, Timothy Peter Thomas. Viongozi hawa mara nyingi wamekuwa wakikataa kushirikiana na wengine , wakiwemo viongozi wa BAVICHA mkoa wakijidai kuendeleza sera ya usomi ndani ya CHADEMA. Mathalani, wote wawili wamekataa kushiriki mikutano iliyoandaliwa na chama mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu na ile iliyoandaliwa mapema na mjumbe wa kamati kuu, Dr. Kitila Kikumbo. Pia, wamekuwa na uhasama kwa muda mrefu hadi kufikia hatua ya kutishiana maisha wao kwa wao, uhasama ambao wengi tunauhusisha na mbio za kuwania ubunge waka 2015 kwani wote wanaonekana wanautaka. Wote waliamua kukwamisha kwa makusudi kabisa mashindano ya BAVICHA wilaya ya Singida mjini mwishoni mwa mwaka jana, mashindano ambayo yaliandaliwa na mwenyekiti wa chama wilaya ya singida nddugu Kumalija. Josephat Isango, ambaye alivuliwa uenyekiti wa BAVICHA kutokana na kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 na baada ya kukmbwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za chama ameendelea kung’ang’ania uongozi na amekuwa akitoa matamko kwa niaba ya viongozi tulioko Singida akidanganya ameyatoa makao makuu ya chama. Timothy Peter Thomas naye, ambaye bado hajakomaa katika siasa za mikikimikiki anasemekana aliilazimisha kamati tendaji ya wilaya ili impe nafasi ya BAVICHA wakati mara nyingi yuko chuoni Dar es salaam na mwaka jana aligombana na Katibu wa wilaya, Yahaya Ramadhani baada ya kukaimu kwa nguvu nafasi ya katibu wa wilaya. Wote wawili pia wamekuwa wakitoa lugha mbaya kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoani hapa akiwemo Katibu wa wilaya, Yahaya Ramadhani. Ndugu Yahaya ameyathibitisha yote haya katika mazungumzo niliyofanya nae wiki iliyopita tukiwa ofisini, Singida.
CHANZO : MIMI MWENYEWE

kabla ya kututaka tukuamini tafadhali thibitisha utambulisho wako (please verify your id)
 
Hivi hujui makao makuu kupelekea hii habari
Jamii forums ndo imekua ofisi ya chadema,hebu pelekeni haya matatizo ofisini tuache unafiki hapa jamvini,umbeya umekua mwingi sana fikisheni makao makuu.
 
Nakushauri usome katiba na sera za chama ndiko utapata ufumbuzi wa matatizo yenu. Vyote utavipata humuhumu kwenye mtandao. Jiandaeni kuongoza nchi si kuumbuana humu JF.
 
Akili yangu inanituma niamini kwamba huyu anatengeneza mgogogro tu wa kipropaganda zaidi. Nafikiri lengo lake ni kuchafua hali ya hewa tu kwani ana uzi mwingine tena anamzungumzia Isango kwamba amekula 1M ya kusaidia wahanga wa vurugu za Ndago. Nahisi huu ni mkakati maalum tu.

Yaani sikuwahi kujua kama CDM wanamzigo mzito hivi. Yaani wamekalia umbeyaumbeya kama wametumwa vile, hawa wangekuwa CCM tungesikia vifo vya presha kwa vijana vingi sana. Waache umbeya wajenge Chama huko
 
Ndugu yangu, huyu mleta uzi amejiunga JF jana na unaweza ukakuta hata si mwanachama wa chadema bali kaamua tu kutengeneza zengwe. Wamo wengi humu JF wa aina yake kwa hiyo usiwe mwepesi kushawishika kwamba huyu ni mtu wa CDM.
 
Malalamiko haya yangepelekwa kupitia vikao rasmi vya chama tungekupongeza sana.
Ni vizuri kila kikwazo kinachogunduliwa kukidhoofisha chama kishughulikiwe kikatiba.
Hapa jukwaani ni kwa uchache sana habari za udhaifu wa CDM hazitafanywa dili na CCM.
 
Back
Top Bottom