Viongozi CWT Kiteto Kitengo cha wanawake wanolewa

Viongozi CWT Kiteto Kitengo cha wanawake wanolewa

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Eng. Tumain Magesa mgeni rasmi warsha ya walimu wanawake wa Chama Cha Walimu CWT iliyofanyika mjini Kibaya.

Akizungumza na walimu wanawake ambao ni viongozi wa Chama hicho alisema walimu ni kioo cha jamii ambacho huigwa kila kukicha.

Alisema jamii ikiona jambo lolote linalofanya na mwalimu huiga kwa dhana ya kuwa ni jema hivyo anapofanya muovu huleta madhara makubwa kwao.

Alisema kimsingi walimu ni waadilifu na kudai miongoni mwao wameanza kukengeuka na kuanza kuchafuka ndani ya jamii.

"Nataka kuona walimu wakiwa kàtika maadili mema kama ulivyo hapo nyuma waache kuiga mavazi yenye maadili mbaya, kwani baadhi yenu mnavaa mavazi ya ajabu..mikono ya sweta mitaani hilo halikubaliki"

Alisema Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada njema za walimu hao katika kulitumikia Taifa kusomesha wanafunzi na hata kuelimisha jamii.

Akisoma risala mbele ya mkuu huyo wa Wilaya Mwenyekiti wa kitengo cha wanawake CWT, Agnes Lyatu, alitaja malengo la warsha hiyo kuwa ni kujenga uwezo wa walimu wanawake katika kukabiliana na changamoto zilizopo maeneo yao ya kazi.

Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na uhaba wa fursa za uongozi katika nyanja mbalimbali za kuchaguliwa au kuteuliwa

Alisema wawakilishi wa Chama Cha Walimu CWT Kiteto ni 105, wanawake 21, Walimu wakuu ni 87 wanawake ni 9, Wakuu wa shule ni 17 wanawake 3, Maafisa Elimu Kata ni 23 wanawake 5.

Alisema idadi hiyo ni ndogo hivyo moja ya sababu ya kukutana viongozi hao wa walimu wanawake ni kujengeana uwezo ili waweze kuomba nafasi mbalimbali za uongozi na kupata kutumikia Taifa.

Hata hivyo alisema walimu wanawake wengi hawajui maadili, sheria na haki mbalimbali za walimu wanawake katika kazi.

Kutojua sheria za ndoa na mirathi, Afya na magonjwa mbalimbali yanayoambukizwa akinamama, maadili ya viongozi na misingi ya uendeshaji ya vyama vya wafanyakazi.

Hata hivyo kitengo hicho kimeanzisha shughuli za ujasiriamali, utengenezaji wa Batiki, Hereni, Mikufu, Bangili, Sabuni, na dawa za chooni.

Kia kitengo hicho kinakusudia kuanzisha kituo cha kulelea watoto wadogo ili kuwapunguzia adha wanawake watumishi ya kuwaacha watoto wadogo bila uangalizi wa uhakika.

Warsha hiyo iliandaliwa na kitengo cha walimu wanawake kinachowakilisha jumla ya wanawake 555 wa shule za msingi Sekondari na Taasisi
 

Attachments

  • IMG-20180907-WA0000.jpg
    IMG-20180907-WA0000.jpg
    15.7 KB · Views: 19
  • IMG_20180907_105245.jpg
    IMG_20180907_105245.jpg
    57 KB · Views: 26
  • IMG_20180907_111042.jpg
    IMG_20180907_111042.jpg
    80.4 KB · Views: 23
  • IMG_20180907_104027_1.jpg
    IMG_20180907_104027_1.jpg
    61.6 KB · Views: 23
  • IMG_20180907_111127.jpg
    IMG_20180907_111127.jpg
    77.6 KB · Views: 18
Back
Top Bottom