figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
SERIKALI imesema tukio la nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa bomu uchunguzi umebaini lilifanywa na baadhi ya viongozi wandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF).
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni amelieleza Bunge mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Gando, Othman Omar Haji.
“Uhalifu wowote utakaofanywa na chama chochote cha siasa au mwanachama serikali lazima ichukue hatua, hata katika suala la nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar kulipuliwa na bomu viongozi wandamizi wa CUF ndio walirusha bomu hilo,”alisema.
Masauni alisema baada ya kukamilika uchunguzi wa tukio hilo, taratibu zinaandaliwa kwa ajili ya kuwafikisha wahusika mahakamani.
Hata hivyo, Masauni hakuwataja majina viongozi wa CUF wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo na Nipashe Digita inaendelea kufuatilia suala hilo kwa undani.Tukio la kulipuliwa nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar lilitokea Machi mwaka jana.
Chanzo: Nipashe