Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Tume iliyoundwa kuchunguza ubadhirifu kwenye chama kikuu cha ushirika cha Songea na Namtumbo(SONAMCU) imebaini ubadhirifu wa shilingi bilioni moja ambapo kutokana na ubadhirifu huo aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya SONAMCU Bw. Philoteus Mbawala anashikiliwa na polisi na viongozi wengine watano kwa tuhuma za ubadhirifu huo.
Mkurugenzi msaidizi wa rasilimali watu wa tume ya maendeleo ya ushirika nchini bw. Kawina Kawina amesema kuwa watu wengine waliotajwa kwenye ripoti hiyo wanaoshikiliwa polisi kwa tuhuma za kuhusika na ubadhirifu wa shilingi bilioni moja ni Hatibu lihonda,Damas Ngonyani,Awadhi Nyoni na Eva Kihwili.
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Pololeti Kamando Mgema amesema kuwa wataendelea kuondoa mchwa wa ushirika ili ushirika mkoani Ruvuma ukae sawa.
Mbunge wa jimbo la Namtumbo ambaye ni mdau wa ushirika mhandisi Edwini Ngonyani amewataka viongozi wa SONAMCU kutafuta ufumbuzi wa malamiko ya fedha za wakulima ili wakulima walipwe fedha zao wanazodai.
Hivi karibuni bodi ya chama kikuu cha ushirika cha Songea na Namtumbo(SONAMCU) ilivunjwa na kuundwa upya kutokana na kukiuka sheria za ushirika.
Chanzo: ITV