Viongozi 11 CHADEMA watiwa mbaroni Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi 11 CHADEMA watiwa mbaroni Dodoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Oct 20, 2011.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Habel Chidawali,Dodoma
  POLISI mkoani Dodoma wanawashikilia viongozi 11 wa Chama Cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) kwa tuhuma za kukiuka amri ya polisi iliyozuia kufanyika kwa mkutano wa hadhara.

  Waliokamatwa ni pamoja na viongozi wa kitaifa wa chama hicho, akiwemo Mkurugenzi wa Opereshi , Benson Kigail na wenzake wa Mkoa na Wilaya ya Dodoma Mjini.Viongozi hao ni Enock Mhembano, Ahmed Sango, Magreth Ttadei, Kundi Yusufu, Alex Nikolaus na Katibu wa wilaya Jera Mambo.

  Orodha hiyo pia inawajumuisha Katibu wa Mkoa Stephen Masawe, Edward Sango na Allid Zoya ambao Polisi walisema wanahitaji maelezo yao ili kujua sababu za kufanya mkutano licha ya kuzuiwa.

  Chadema waliomba kibali cha kufanya mkutano huo jana katika Viwanja vya Barafu, lakini polisi walizuia bila ya kueleza ni lini mkutano utafanyika.

  Oktoba 16 mwaka huu, uongozi wa Chadema katika Wilaya ya Dodoma uliindikia polisi, kuomba kufanyika kwa mkutano huo lakini jana polisi ilipeleka barua ya kuuzia, saa chache kabla ya kuanza.Hata hivyo viongozi hao walikusanyika katika uwanja huo, hatua iliyowalazimisha polisi kuwakamata na kuwashikilia.

  Hali hiyo iliwalazimisha wanachama wa Chadema, kukusanyika katika kituo cha polisi wakitaka kujua sababu za kuzuiliwa wa mkutano huo.

  Kitendo hicho kiliwalazimisha polisi kuimarisha ulinzi

  “Sisi tulipeleka barua ya kuomba kibali cha kufanya mkutano wa hadhara katika eneo hilo na kila taratibu tulizifuata lakini cha ajabu leo (jana) saa 5:20 asubuhi tukapokea barua ya kuzuia mkutano saa chache kabla ya kuanza. Tunashangaa kweli,’’alisema Idd Kizota ambaye ni Katibu Vijana wa Wilaya.

  Katibu huyo alisema lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuhamasisha wananchi kujiunga na chama hicho na kuhimiza umuhimu wa kuimarisha matawi ya chama.Barua iliyoandikwa na polisi kuzuia mkutano huo, ilisema hatua hiyo imetokana na sababu za kiusalama na haikueleza ni lini utafanyika tena.

  Mmoja wa viongozi wa polisi wilayani Dodoma ambaye hakupenda jina lakelitajwe kwa madai kuwa si msemaji, aliliambia gazeti hili kuwa Chama walifuata taratibu zote zilifuatwa, lakini hatua za kuuzuia mkutano huo zimetokana na habari za ndani kuhusu nia ya mkutano huo.

  Viongozi 11 Chadema watiwa mbaroni
   
 2. B

  BMC Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 5
  chama cha dampo na magereza!
   
 3. u

  ureni JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,273
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  CCM wangewaacha tu waendelee na mkutano wao,manake kwa staili hii ya kuwanyanyasa,kuwazuia wasifanye mkutano na kuwakamata na kuwaweka mbaroni wanakua wanazidishia kuipa umaarufu CDM.Nakumbuka kuna mkutano wa UVCCM ulifanyika Arusha bila kibali lakini hawakuguswa na wala mkuu wa polisi hakusema ni hatua gani atakayowachukulia alipotezea kiaina,kweli TZ hamna haki kabisa.
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Acha waendelee hivyo hivyo ndiyo changamoto za kukabiliana nazo hizo, na hakika zitawafanya wanaCDM waendelee kubuni mbinu nyingi zaidi za kuweza kupatia ufumbuzi wa hizi fitina. Kama CDM watatumia vizuri hizi fursa za kihujuma, basi wanaweza kushinda hii vita kwani matatizo yeyote huwa ni fursa nzuri ya kujifunza kwa kutafuta majibu yake.
   
 5. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  usalama upi?jaman toka lini wagogo wakaleta vurugu?mbna polisi wanachekesha?
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndiyo dalili nzuri ya UKOMBOZI. Viva CDM!!!!
   
 7. m

  muafaka Senior Member

  #7
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nyie wanasiasa mna matatizo sana!, mnaponadi masuala yenu mnataka tuwaamini na tunafanya hivyo kwa kutambua nafasi ya siasa katika jamii.
  SWALI: Kwa nini hamtaki tuamini taarifa zinazotolewa na taasisi nyingine zenye wajibu wa kikatiba kama Polisi? Au tuseme nyie ni malaika zaidi?
   
 8. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,472
  Trophy Points: 280
  ccm hawataki kung'oka eneo la mjengoni,iliwauma jinsi walivyong'oka Arusha mjini,2015 kitakachotokea ccm hawataamini.
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  CCM wanashangaza sana UVCCM,Katibu mwenezi anafanya mikutano mahala popote na wakati wowote anaotaka,,Hivi Polisi na CCM wanadhani nchi ni yao peke yao ,hii ni mbaya kutwa kudharilisha viongozi wa Chadema sio tabia nzuri kwa musitakabali wa taifa letu,waache chuki na chama cha Chadema wamezidi sasa Polisi utafikili hawakuenda shule
   
 10. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sijui hii serikali itajifunza lini?????? Inafahamu kabisa kama kuwakamata kamata viongozi hao bila sababu za msingi ndo wanawaongezea umaarufu lakini hawasikii.
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,026
  Likes Received: 745
  Trophy Points: 280
  Kivipi mkuu?
   
Loading...