Vioja Katika Daladala!

Bazazi

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2008
Posts
2,806
Reaction score
3,502
Kwa wale wenye magari na kwa kawaida hampandi Daladala;
Hivi ndivyo viroja tunavyopata kwenye Daladala wenzenu tusio na magari




Mlokole: "Nyimbo gani mnapiga?!? Wekeni nyimbo za Yesu.."
Konda: "Vipi wewe, Yesu bado hajatoa album..."
********************************
Abiria: "Kuna Kiti au unasema panda tu!?"
Konda: "hao wengine wamekalia ndoo?! "
*******************************
Abiria: "Embu punguzeni sauti ya redio..."
Konda: "Sheria za nchi tu zinatushinda, tusikilize na zako!? hebu tupunguzie misheria"
*******************************

Mmama: "Bwana ondoa gari joto sana!!"
Konda: "Usituzingue wewe, shuka upande fridge...."
******************************
Konda: "Anti, kuna siti pale nyuma, ingia...."
Anti: "Siwezi kaa siti za nyuma..."
Konda: "Kwenda zako wewe, Kwani za nyuma ziko nje ya gari?!"
********************************
Sister duu: "Konda unanibana bwana..."
Konda: "mbona nguo ulizovaa huzisemi, kama ulitaka kujiachia ungekodi treni peke yako!!!"
*******************************
Sharobaro: "Kuna kiti?! Kama hamna sipandi..."
Konda: "Kama unaogopa kukosa kiti si ungebeba chako!!?"
 
Konda: Naomba nauli..
Abiria: Kwani hujapewa NYUMA??

Konda: we shoga nini, nani kakwambia anataka 0714 yako hapa...
 
Daladala zina kero ila wakati mwingine zinafurahisha sana maana utasikia maneno ambayo maishani hujawahi kuyasikia na hutoyasikia tena
 

Epuka kauli zifuatazo uwamo ndani ya daladala, Nitakupa,Atakupa mbele,Hujapewa mbele?,Utapewa nyuma,Nitakupa nikikaa vizuri,Ngoja isimame nikupe,Subiri asimamishe nikupe n.k ongeza nyingine tata.
 
Abiria:konda wa2 wamejaa usipakie wengine.
Konda:gari halijaagi,chupa ya chai ndio inajaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…