vinauzwa viwanja - Mbezi/Kibamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

vinauzwa viwanja - Mbezi/Kibamba

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Landed Property, Nov 19, 2011.

 1. L

  Landed Property Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanaJF
  Vipo viwanja sabini vyenye ukubwa wa sqm 700, 900, 1200 eneo liitwalo Kwembe. Ni 3km kamili kutoka morogoro road upande wa kushoto kama unatokea DSM. Viwanja vimegawanywa na mmiliki wa eneo kwa kuweka barabara za kutosha, havina hati ya wizara ila ni halali kwa makazi. Bei ni kuanzia shs 4m. Ukipenda na uwezo unaruhusu unaweza kuviunganisha hata vinne sehemu moja.
  NOTE; mimi sio muuzaji wala dalali ila ni mkazi wa jirani na eneo hilo hivyo nimeamua kuwashirikisha ili kuwasaidia wanaohitaji.
  Asante
   
 2. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  tunashkuru kwa taarifa
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  salutation for you
   
 4. K

  KASRI Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tafadhali tupe contacts za mhuusika tufanye bizness
   
 5. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,034
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Wanajamvi kuwekeza katika ardhi ni muhimu sana lakini chukueni tahadhari kubwa eneo hilo lina mgogoro sana na pia kuna kesi mahakamani

  Google ardhi Kwembe halafu soma kwenye link: Mgogoro wa Kwembe watua kwa Pinda - Bwagamoyo

  Sisemi kila eneo Kwembe lahusika lakini km alizotaja toka Moro road likpo kwenye mradi
   
 6. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,087
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu, ila kuna

  PAGALE; lenye ramani ya kisasa (1masterroom, 2beding room, 1 seating room, 1 dinning room, smallstore and a public toilet)

  LOCATION; kunduchi mtongani( njia panda ya wet n world), ni ya pili kutoka barabarani

  BEI;25mil(haina dalali)

  CONTACTS; 0714 581449(Joshua)

  "KARIBUNI NYOTE"
   
 7. L

  Landed Property Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeah!
  Ni kweli eneo la mradi kwembe linamgogoro ILA eneo nililolitaja lipo nje ya mradi. Eneo la mradi limeishia Block A Kwembe. Sehemu yenyewe inaitwa maduka sita, ni jirani na ofisi za serikali ya mtaa. Ukihitaji maelezo zaidi unaweza kuulizia ofisi ya serikali ya mtaaa au wizarani au Kinondoni manisipaa kujihakikishia kutokuwa na mgogoro.
  Nasisitiza kwa serious b mtu anayehitaji eneo hilo hana haja ya kuogopa. Ninaishi jirani na eneo hilo, mgogoro wowote ningeufahamu na nisingependa nione watu wanatapeliwa au kusababishiwa mgogoro maana sitafaidika na chochote sana sana nitaathirika na mimi
  Just go and see the place
   
 8. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Asante kwa taarifa mkubwa. kwa anayekihitaji ni vizuri kujiridhisha na angalizo lililotolewa hapo juu.
   
 9. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tahadhari ni muhimu. Thanks Mkuu.
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,151
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Mmmmhhhh mbona twatishana na mgogoroooo haya msionavyo viwanja changamkieni ila kuweni makini viwanja vingi vya wilaya ya k/ndoni na ilala vina migogoro
   
 11. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nijuacho ni kwamba Kwembe kuna migogoro ya ardhi, labda kama mgogoro umeisha. Binafsi nilikuwa na kijieneo changu huko na nafahamu kilichokuwepo huko.
   
 12. Nemo

  Nemo JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 661
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 80

  Mgibeon

  Unaweza kunielimisha Pagale ni nini? Msingi wa nyumba ulioanzwa or nini ? Na Pia ukubwa wa kiwanja je? picha if possible pls!
   
 13. L

  Landed Property Member

  #13
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa za jana toka kwa dalali mmojawapo (Shabani) wa viwanja hivyo na mimi mwenyewe nilifika hapo kwenye viwanja;
  Vimenunuliwa zaidi ya 50% tayari na jumamosi walionunua walikuwa wanajengea mipaka vizuri.
  I wish ofisi za ardhi zingewashawishi watu wenye maeneo wanayouza (ambayo hayajapimwa) wafanye kama huyu bwana alivyofanya ---- yaani amevigawa viwanja vizuri, amechonga barabara zenye upana wa kutosha.... nimesikia alishirikiana na afisa ardhi/mpimaji wa ardhi mmoja (tetesi) kuvigawanya. Hakika eneo kama hili sitegemei kuona mwonekano kama wa baadhi ya maeneo ya uswahilini ambapo hata kiwanja cha sqm 100, 80, 150 unapata kisha hata mkokoteni hauna njia.

  Karibuni Kwembe tujenge mtaa wetu
   
 14. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,087
  Trophy Points: 280
  Mkuu, pagale ni jengo lisilokamilika.. Kwa kesi iliyopo hapo ni kwamba mjengo huo upo ktk "renta" ikimaanisha bado " kozi" mbili uanze upauzi..! Ukubwa na picha sijafanikiwa kuuliza, kupaona hapo site ni bure kabisa ni uamuzi wa kumpigia huyo Joshua atakupeleka..!
   
 15. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,034
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Kama vipo upande wa kulia sambamba na Maduka sita (kama unatoka Serikali ya Mtaa kwenda mjini) basi vipo salama lakini upande wa kushoto ogopa sana kwani kuna mgogoro mkubwa pale kwani watu wa ardhi wlipima eneo hilo kihuni wakiwalipa watu wa kudadikika na hivyo kupelekea mgogoro. Pia kuna kiwanja cha Kanisa la SDA wao wana ekari kama 22 hivi hivyo ukiingia kichwa kichwa wale ni Radical sana watakuondoa tu.
  Upande wa kushoto ni salama mwenyewe ni Afisa Ardhi wakati wa mradi alipakwepa makusudi kwa nia labda ya kuuza baadaye kama ni yeye anauza Okay nunueni kwani ni kwake (Yaani pale kwenye container la celtel)

  Mimi nakaa maeneo hayo na nimeshuudia watu wakiuziwa migogoro kwa bei kubwa sana
   
 16. S

  Speedo Member

  #16
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 13
  Bwana Nyati,

  asante kwa kutoa taarifa zaidi.
  mimi Binafsi baada ya kusoma post ya kwanza jumamosi nilifika eneo husika.
  1. Nimeonyeshwa eneo linalouzwa - lipo upande wa kulia baada ya maduka sita kama unaenda serikali ya mtaa kutokea mjini.
  2. Ni eneo linalopakana na eneo lililopimwa la mradi (Block A kwembe).
  3. Eneo linapakana na eneo la Kanisa SDA (upande wa Kusini), wamiliki wengine pande za Magharibi na Kaskazini, Barabara kubwa ya Kwembe (Mashariki).

  Ni kweli eneo linasemekana halina mgogoro na baada ya kuwasiliana na rafiki yangu from ministry of Lands amenieleza kuwa eneo hilo lilipimwa zamani sana kama shamba ila halitambuliki tena kama limepimwa hivyo lipo free kwa yeyote kujipimia akipenda ila ni kwa ajili ya makazi.

  Kwa kusikia hivyo nilijikuta nashawishika kununua na asubuhi ya leo nilitoroka kwa mwajiri na hapa nimetoka kulipia viwanja viwili - sqm 1200 @ Shilings 7.5m.
   
 17. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,034
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  HONGERA SANA na KARIBU KWEMBE. Katika maelezo yako umejiridhisha kuwa angalau kwa asilimia 99.99999% hata mimi sina maswali zaidi hapo ila juu ya hiyo Block A, ni ya mradi upi? kwani mradi wenye mgogoro una blocks nne (Kitalu 1 hadi 4) Block 1 ni karibu na shule ya Babro Johansen, Block 2 ni karibu na Container kwa itandula, Block 3 ni maeneo ya Maduka matatu, Block 4 ni pale kulia kwa Maduka sita. Hivyo labda lipo jirani na Block 4.

  Pia kuna barabara ya mita 70 kwenda kwenye mradi wa Muhimbili

  Hata hivyo karibu sana, nitaanzisha vikao vya wan JF Kwembe, Kibamba na Luguruni pale La Paz hivi karibuni. By the way wengine wajue kuwa karibu na hapo kutakuwa na mradi wa Chuo kikuu cha Muhimbili, Chuo cha St Joseph na mji wa mfano wa Luguni hivyo eneo linapanda value haraka sana
   
 18. L

  Landed Property Member

  #18
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndg Nyati,
  Naungana nawe kumkaribisha speedo Kwembe.

  Hata hivyo naomba msaada wako kujua hiyo barabara ya 70m inapitia wapi? Japo mimi nipo huku serikali ya mtaa. Je! Ni kutokea pale maduka 6 kwenda Muhi2 kupitia kwa bw. Sulle (mkwe wa former PM) au ni sehemu nyingine?
   
Loading...