Vimemo Bandarini; Nani walikuwa wanaandika?

Kadi ya kupambana na ufisadi haiwezi kufanyika kikamilifu na chama kilekile ambacho makada wake ndio watuhumiwa wakubwa wa ufisadi. Sababu ni kwamba ukichimbua sana lazima viongozi wengi wakuu wa serikali iliyopita watakuwa implicated! Hapa ndipo Magufuli atakwama na kubaki kuhangaika na vidagaa.
Hii kazi ingeweza kufanyika vizuri zaidi km chama kingine kingeingia madarakani kwa ssbabu hakungekuwa na kuoneana aibu!
 
Watu kulalamika hata kisicho na kweli,
Yeye kama rais alisema waliokwepa kido waende wakalipe,majina ya watumishi waliotumia nafasi zao kusaidia watawajibishwa
So suala la vimemo aliyeandika kimemo na alikipokea watajuana sisi tunataka kodi zetu
Ina maana aliyekwepa analipa tu kodi na hakuna hatua zingine kwa kosa la kukwepa kodi? Hapo itakuwa sawa na riwaya ile ya EPA
 

Ni kweli watu wanatumia nguvu nyingi neno "vimemo" lisikumbushwe.
 
Mh! huu utaratibu wa sasa mie nawasiwasi nao mie nafikiri kuwafukuza vigogo kazi haitoshi! na mpunga wetu waliokula walipe kwan wanajua walipopeleka.
 
Wahusika wanatakiwa kulipa ushuru wa makonteina yao nukta. Mambo ya vimemo, kama walivinunua au kutoa rushwa watajuana wenyewe kwani mtu hawezi kupindisha taratibu na sheria kwa vimemo.

Good, mkuu sheria zipo na mhusika ambae ni mtaalam kapindisha sheria kwa vimemo, wataalam wa namna hiyo waendelee kupokea vimemo na tutaendelea kuwafunga/kuwafukuza kazi.
 

Hivi bongo hatuna watu wenye principle za kukataa vimemo na hata kujiuzulu kama wanaamrishwa tofauti na sheria?

Kusema niliandikiwa kimemo si utetezi.
 
vidagaa tu vitakurupushwa mapapa na manyangumi miguu juu kwa mbele
 

Mkuu vimemo vingine vya kuhuni, yani hakina tarehe wala sahihi au ni feki wewe mtaalamu umeenda shule unapokea kimemo bila kuhoji then utoa makontena tu shauri yako na hayo mamemo utafungwa sababu mwenye memo mwenyewe atakukana na utaua familia yako
 
huo mziki ndio mtajua kwamba,ccm ni ileile ya kulindana labda yawe majina ya wapinzani lakiini kama ni ya wana ccm itakuwa ndoto

Mkuu gogo la shamba.. Wapinzani wataandikaje vimemo wakati hawana serikali?
 
Hivi bongo hatuna watu wenye principle za kukataa vimemo na hata kujiuzulu kama wanaamrishwa tofauti na sheria?

Kusema niliandikiwa kimemo si utetezi.
Kiranga kama hakuna hata kiongozi mmoja anayeboronga na kujiuzulu itakuwa mtendaji ajiuzulu kwa sababu kapewa kimemo cha kumuagiza afanye jambo ambalo yeye hakuridhika nalo kwa vile limekwenda kinyume?
Hiyo sio Tanzania hii labda iwe nchi nyingine. Ukigoma na kufukuzwa kazi au kufanyiwa mizengwe mingine hakuna hata mtu mmoja atakaye kutetea wala kukupongeza zaidi ya kejeli ndio maana wengi wanasema potelea mbali.
Kumbuka yule Mwanasheria wa Tanesco na mkataba wa PAP na IPTL yaliyomkuta.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu vimemo vingine vya kuhuni, yani hakina tarehe wala sahihi au ni feki wewe mtaalamu umeenda shule unapokea kimemo bila kuhoji then utoa makontena tu shauri yako na hayo mamemo utafungwa sababu mwenye memo mwenyewe atakukana na utaua familia yako

Mkuu tunataka kuwajua hao waliokuwa wanawalazimisha watumishi watendaji kukiuka sheria. Tuwajue maana isije kuwa wengine bado wana madaraka makubwa au wanafikiriwa kupewa Uwaziri nk nk. Hata kama mahakamani havitakuwa ni solid evidence lakini ni msaada kuelewa mengi na kukomesha mengine siku zijazo toka kwa hao watoa vimemo.
 
Nashukuru Mungu mpaka jana 8billion kati ya 12 bilion ishaingia kwa Magufuli a.k.a serikalini kwahiyo bibi yangu kule Mliayoyo atapelekewa madawa ya kutosha kwa bei nafuu. Endeleeni kubishania makaratasi (memo) yeye Msukuma anaikimbiza shilingi hapa kazi tu.
 
Tatizo ni Katiba ndugu zangu, kwa mfumo wa Nchi hii vimemo vitaendelea kufanya kazi tu.

Mfano mzuri ni ndani ya Jeshi la Polisi na Majeshi yetu yote kwa ujumla, Hivi kwa askari mwenye cheo cha koplo ana jeuri gani ya kukataa kimemo kilichotoka kwa askari mwenye nyota moja?

Mfano mzuri ni Askari wa Usalama Barabarani ni wangapi wamevuliwa Uniform zao nyeupe na kupelekwa kulinda mabenki kwa kukamata gari ya hawara wa Kigogo wa ndani ya Jeshi la Polisi au Serikalini hata kama lina makosa ya wazi?
 

Hapana mkuu, hapo utakuwa hujatenda haki na bado utakuwa unaendeleza ubabe uleulea wa miaka yote wa kuwaacha mapapa na kudili na vidagaa , kiukweli kama kweli kuna haki inatendeka basi wote waliokubali na waliotoa vimemo watajwe wazi na hukumu zao ziende sambamba na hawa maofisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…