Vilinge vilivyothibitishwa maeneo mbalimbali nchini

Naomba uzi huu uwe natija kwa wote watakao itaji huduma kutoka kilingeni. Na wale ambao wataleta habari sijui za yesu, Mungu na wengine mara sijui nini, huu uzi sio wao maana hayajawakuta.

Naomba nimpe pasi honorable Dr Mshana Jr awezeku-share nasi vilinge mbali mbali anavyovifahamu kutoka katika kila kanda, mkoa, wilaya ya nchi bila kusahau jina na kijiji.

UPDATES KUTOKA MALEGENDARI

01. Kwansisi Handeni Tanga
02. Mapango ya Amboni Tanga
03. Majani mapana Tanga
04. Ludewa njombe vijiji vya Mundende, ibumi, ludende au nenda sehemu inaitwa JIWE LIGANGA

05. Kiwila, ngosi ziwani
06. Mwamboni Tanga
07. Vudee Same
08. Tukuyu Ushirika kijiji cha Utete ( nasikia mtaalam wa hapa ni tapeli)
09. Weruweru... Hai Kilimanjaro
10. Chitipa, mpakani mwa Ileje na Malawi na Zambia.

11. Mwandoya Bariadi - nasikia mpaka helicopters zikiwa na waheshimiwa uwa zinatua huku

12. Liwale, kuna kijiji kinaitwa Ngende.

13. simiyu Longa Lombogo
14. Kijiji cha Ikungulyabashashi kipo bariadi unashukia senta ya nyakabindi

Nitaendelea kuongeza kadili vilinge vinavyozidi kutambulishwa wachangiaji.

Na wewe unaefahamu machaka yanayotoa huduma zilizonyooka unakaribishwa pia kuchangia.

Mimi nimekaa pale nachukua notisi.
 
Mundende,ibumi,ludende au nenda sehemu inaitwa JIWE LIGANGA(hapa liganga,mkoroni alifichaga mali lakini aliporudi kuzichukua akarogwa na hazijawahi tolewa)
Hivi kumbe mali zikifichwa kichawi ni ngumu kuzitoa/kuziona? JE nikileta greda litifue ardhi haziwezi onekana? Au hii sayansi imekaaje?
 
Hivi kumbe mali zikifichwa kichawi ni ngumu kuzitoa/kuziona? JE nikileta greda litifue ardhi haziwezi onekana? Au hii sayansi imekaaje?
Hata zile story za kaburi katikati ya barabara(iringa) ni kweli...na ukitaka uhakika waulize TANROAD
 
Hata zile story za kaburi katikati ya barabara(iringa) ni kweli...na ukitaka uhakika waulize TANROAD
Lile kaburi nalijua maana lipo karibu na kijiji chetu cha njia panda ya mlolo ni dakika 15 tu toka kijijin na lile kabuli maana yule mzee ni wa maeneo yale.
 
Walokole mnatakiwa kuvijua hivi Vilinge! Hivi ni Viti vya Enzi vya SHETANI! Na mnatakiwa kuvibomoa katika maombi!
 
Sumbawanga na kigoma hawana mbwembwe. Ila ukienda ndio utajua.
Ziwa Tanganyika ndio nguzo kuu inauounganisha Sumbawanga kihoma na kongo.
Kisha unaenda kufuata bonde la kati mpaka Niger huko ndio chanzo kikuu cha mtu mweusi na maajabu yote ya mwafrika. Ogopa kigoma kule kuna mafundi.
Naishi nyanda za juu kusini watu pekee ukanda huu ni wakinga walau wanajaribu, jaribu nikilinganisha na nyumbani maghaibi na usukumani, huku bado sana.
Wapangwa wao wanasifiwa kwa kuoga tu na si tiba kwa jumla wake.
Mimi kama mtu wa kutoka bonde la Tanganyika mtu anaweza kumuogopa ni msukuma. Wasukuma wanajua tiba sana sana.
Bora umetoa shot out kwa wakubwa zako.

Nasikiaga majina kama wakinga, wasambaa and the like eti.

In short shukuruni tu wasukuma hatunaga roho mbaya kama wachaga.
 
Naomba uzi huu uwe natija kwa wote watakao itaji huduma kutoka kilingeni. Na wale ambao wataleta habari sijui za yesu, Mungu na wengine mara sijui nini, huu uzi sio wao maana hayajawakuta.

Naomba nimpe pasi honorable Dr Mshana Jr awezeku-share nasi vilinge mbali mbali anavyovifahamu kutoka katika kila kanda, mkoa, wilaya ya nchi bila kusahau jina na kijiji.

UPDATES KUTOKA MALEGENDARI

01. Kwansisi Handeni Tanga
02. Mapango ya Amboni Tanga
03. Majani mapana Tanga
04. Ludewa njombe vijiji vya Mundende, ibumi, ludende au nenda sehemu inaitwa JIWE LIGANGA

05. Kiwila, ngosi ziwani
06. Mwamboni Tanga
07. Vudee Same
08. Tukuyu Ushirika kijiji cha Utete ( nasikia mtaalam wa hapa ni tapeli)
09. Weruweru... Hai Kilimanjaro
10. Chitipa, mpakani mwa Ileje na Malawi na Zambia.

11. Mwandoya Bariadi - nasikia mpaka helicopters zikiwa na waheshimiwa uwa zinatua huku

12. Liwale, kuna kijiji kinaitwa Ngende.

13. simiyu Longa Lombogo
14. Kijiji cha Ikungulyabashashi kipo bariadi unashukia senta ya nyakabindi

Nitaendelea kuongeza kadili vilinge vinavyozidi kutambulishwa wachangiaji.

Na wewe unaefahamu machaka yanayotoa huduma zilizonyooka unakaribishwa pia kuchangia.

Mimi nimekaa pale nachukua notisi.
Sumbawanga siioni hapo.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Milima ya ukinga huko makete umeshawahi kuisikia? Hao wanaotaka kusaidika wanaweza kula maini mabichi yanayovuja damu?,wanauwezo wa kuamka kila siku saa nane kuviachia vitu vikasafishe njia?
Acha kutuchafua huo ni uongo 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom