Vikwazo uchumi wa viwanda vyatajwa

Vikwazo uchumi wa viwanda vyatajwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Wakati Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, ikipokea taarifa za makosa ya rushwa 163 kwa mwaka wa fedha 2016/17, imeelezwa kuwa vitendo hivyo vitakwamisha lengo la Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Vilabu vya wanafunzi wa kupinga rushwa walisema hayo juzi walipohudhuria mdahalo usemao “Rushwa inavyoathiri Maendeleo ya Uchumi na Viwanda,” na kuongeza kuwa Takukuru bado ina kazi ya kuelimisha umma kuhusu vita hiyo.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari Buhongwa, Jaquline Changu pamoja na kumpongeza Rais John Magufuli kwa hatua anazochukua kwa wala rushwa, alisema ili nchi ifikie maendeleo ya uchumi wa kati na viwanda ni lazima vitendo hivyo vidhibitiwe.

“Mfano mtu anaajiriwa kwa kutoa rushwa ya ngono au pesa na wakati huo hana uwezo wala taaluma yoyote ya kazi hiyo, hataweza kufanikisha maendeleo kusonga,” alisema Changu.

Wakiainisha vikwazo vinavyokwamisha maendeleo ya viwanda walisema ni pamoja na kupoteza nguvu kazi ya watu wenye uwezo wa kupeleka maendeleo mbele, kushuka kwa pato la Taifa, ujenzi wa miundombinu usioridhisha, uingizwaji wa vifaa duni pamoja na uvushaji haramu wa nyara za Serikali.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Buswelu, Elisha Peter alizitaja sababu zinazokwamisha maendeleo ya uchumi na viwanda kuwa ni, kukosekana kwa sera elekezi katika viwanda.

Pia, alisema sheria zinazowekwa kwa wawekezaji ni miongoni mwa vikwazo vinavyokwamisha viwanda kutojengwa au kufa.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale alisema taasisi hiyo iliamua kuanzisha vilabu vya kupiga vita rushwa kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu na hadi sasa jumla ya vilabu 147 mkoani mwanza vimeelimishwa kuhusu madhara ya rushwa.

mwananchi
 
Back
Top Bottom