Vikundi hivi vimesajiliwa wapi na kwa sheria ipi?

Vikundi hivi vimesajiliwa wapi na kwa sheria ipi?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,646
Reaction score
164,798
Umekuwa kama ni utamaduni wa kawaida tu kwa watu mbalimbali siku hizi kubuni vikundi na kuvipa majina kama vile "friends of Lowassa" n.k na kisha ku-print t-shirts na vikundi hivi kufanya kazi kwenye jamii yetu kama vile kutoa misaada kwa watu na Taasisi mbalimbali zinazohitaji misaada n.k.

Ok,it's fine!Lakini je,kwa mfano,kesho na keshokutwa, "Salary Slip" nae akaibuka na kikundi chake na kukiita "opponents of the union" itakuwa ni kosa?Kama ni kosa;je, ni kosa kwa sheria ipi ya nchi?Kama kikundi changu kilitakiwa kusajiliwa,ningekisajili kwa sheria ipi?

Au,kwa mfano, nikaamua ku-print t-shirt kadhaa zenye ujumbe "opponents of the union" na kwenye kikundi chetu tukaamua kuzivaa na kuzisambaza nchi nzima itakuwa ni kosa?Kama ni kosa,kwa sheria ipi?

Kumbuka ujumbe unasema tu oppenents of the union bila kutaja ni unioni ipi hasa na watu wa kikundi husika wakaamua kuvaa hizo nguo na kudunda mtaani utawakata na kuwashitaki kwa sheria gani?Hapo ndipo unapokuja umuhimu wa kusajii vikundi vya aina hii.

Au hata nikanzisha kikundi wakati huu ambapo campaign hazijaanza na ku-print t-shirt za kikundi changu zenye ujumbe unaosomeka "opponents of the new proposed constitution" utanibani kwa sheria ipi ili hali kikundi changu hakijasajiliwa na wala sijaitaja hiyo new proposesd constitition ni ipi na ni ya nchi gani.

Zingatia huo unakuwa ni ujumbe tu unaovaliwa na wanakikundi bila kufanya harakati zozote zenye kuonyesha kukiuka au kuvunja sheria za nchi.

Haya mambo kuna umuhimu wa kuyatazama kwa mapana na marefu yake tusingoje mpaka siku yatokee tusiyoyatarajia ndio tuone umuhimu wa kuyatungia sheria au kuyawekea utaratibu.

Wanasheria mtusaidie hapa kwani ingawa mimi si mwanasheria,ila naona kuna "loophole" kubwa tu katika sheria zetu na ambayo imekaa vibaya na tena si kidogo.
 
hao wanatoa njaa tumboni na kupeleka kichwani mwisho wa siku waharibu akili

Jana nimeona kupitia ITV kikundi cha friend of Lowasaa wakiwa wamevalia t-shirt zao za sare na picha ya Lowassa wanatoa misaada kwenye jamii nikabaki najiuiliza maswali mengi bila kupata majibu.

T-shirts za aina hii zinafaa kuandaliwa na kuvaliwa kwenye shughuli maalumu kama vile misiba n.k lakini sio kwa "uholela" huu tulionao sasa ipo siku zitaandaliwa t-shirt zenye ujumbe tusioutarajia kama nchi na tukashindwa kuchukua hatua hasa ujumbe huo ukiandikiwa kijanja kijanja na kitaalamu.

Nimekumbuka na zile t-shirt za Kakobe na waumini wake ingawa binafsi nilizifurahia.
 
Uvivu wa kufikiri na kufanya kazi. Sasa ujumbe wa T-SHIRT aliyovaa mtu unakukera nini. Nawe tengeneza ya kwako. Mbona kuna watu wanavaa T-Shirt za changua Kikwete, Chagua CCM mbona hujawahi kusema hawa wamekosea. Kwani sasa hivi ni wakati wa uchanguzi? Hawajui kuwa CCM na rais Kikwete ndo wametufikisha hapa....sasa ukiona mtu anawashabikia si bora akamatwe. Rudi Nyuma kumbuka ulipoangukia UKATUBU.
 
Njaa ndio chanzo cha hivyo vijigenge vya wachumia tumbo
 
Uvivu wa kufikiri na kufanya kazi. Sasa ujumbe wa T-SHIRT aliyovaa mtu unakukera nini. Nawe tengeneza ya kwako. Mbona kuna watu wanavaa T-Shirt za changua Kikwete, Chagua CCM mbona hujawahi kusema hawa wamekosea. Kwani sasa hivi ni wakati wa uchanguzi? Hawajui kuwa CCM na rais Kikwete ndo wametufikisha hapa....sasa ukiona mtu anawashabikia si bora akamatwe. Rudi Nyuma kumbuka ulipoangukia UKATUBU.
Kuna siku watu watu wata-print t-shirt zenye ujumbe kama huu "I dislike UKAWA","I dislike CHADEMA", "I hate CCM","I hate union of Tanganyika and Zanzibar" n.k.Niambie tutakuwa salama?

Neno " hate" au "dislike" ni kosa kisheria?

Leo hii tuna ujumbe/kikundi "friend of Lowassa",kesho je?
 
Na zileza "I love New York" au michigan au hata za Obama utasemaje mkuu?
 
Na zileza "I love New York" au michigan au hata za Obama utasemaje mkuu?
Ujumbe mzuri una shida gani?

Siasa zetu zinaelekea kubaya sana.

Unakumbuka mbwa alivalishwa bendera ya chama chetu tena hadharani mchana kweupe?

Amani yetu hii ni kwa neema tu.
 
Back
Top Bottom