Vikombe: Janga jipya la kitaifa!!!...................

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
216
Anayetoa kikombe arukwa na akili

na Joseph Malembeka, Morogoro

MGANGA aliyeibuka hivi karibuni akitibu magonjwa sugu kwa kutoa kikombe cha dawa katika kijiji cha Muhola, kata ya Ifakara wilayani hapa Idd Juma (34) juzi alizua kizaazaa baada ya kurukwa na akili na kuanza kufukuza watu hovyo.
Hali hiyo ilisababisha akamatwe na kukimbizwa katika hospitali teule ya Mt.Francis mjini hapa.
Juma ambaye aliibuka Mei 28 na kutangaza kuoteshwa dawa hiyo kisha kuanza kutoa kwa kipimo cha kikombe kwa mwenye magonjwa sugu kama kisukari, kichaa, mapepo na ukimwi alikumbwa na swaibu hilo alfajiri Juni 9.
Mdogo wa mganga huyo, Rashid Kilala alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa dalili za tatizo hilo zilianza kuonekana Juni 6 ambapo alianza kuzungumza maneno yasiyoeleweka mfululizo bila kupumzika.
Akitoa historia fupi ya kaka yake huyo, Kalala alisema awali alikuwa mkulima na mfanyabiashara wa kuku wa kienyeji soko kuu la Ifakara kabla ya kuanza ya utabibu, mwaka 2008 aliwahi kuwaeleza ndugu zake kuoteshwa na malaika kuwa atakuwa na kipaji cha kutibu watu magonjwa sugu.
Alisema kabla ya kupata matatizo hayo kaka yake huyo ambaye alitoa dawa hiyo pasipo kiwango malumu cha malipo tayari alikuwa ametoa kikombe hicho kwa zaidi ya watu 1,500 kutoka maeneo mbalimbali ya wilayani humo.
Aliongeza kuwa kadri siku zilivyosonga mbele alianza kumchukia mdogo wake huyo na nduguze wengine huku nyakati za usiku akionekana kukosa usingizi kwa kufanya maombi usiku kucha.
"Ilipofika Juni 9 alfajiri nikapigiwa simu na majirani na kuelezwa kuwa kaka yake amerukwa na akili na anakimbia hovyo mitaani huku akiwatisha watu kuwapiga na kusema kuwa anaelekea benki kuchukua fedha zake wakati akielewa kuwa hana akaunti katika benki yoyote," alisema na kuongeza.
Nikaanza kumfuatilia na kumkuta kweli akikimbia mitaani na kulazimika kupiga simu kituo cha polisi ili kupata msaada ambapo tulimkamata na kumfikisha hospitali."
Juhudi za kumpata mganga wa hospitali hiyo Dk. Anthony Magoda kuzunguzia zaidi tatizo hilo zinaendelea.

chanzo: tz daima

 
Back
Top Bottom