Viko wapi vitabu vya makadirio ya Bajeti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viko wapi vitabu vya makadirio ya Bajeti?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Scan, May 31, 2012.

 1. S

  Scan Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taarifa Kwa Vyombo vya Habari, Jumanne, 29 Mei 2012
  Viko wapi vitabu vya makadirio ya Bajeti?
  Tumesikitishwa na hatua ya Serikali kushindwa kutoa vitabu vya makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2012/2013, siku 21 kabla ya kikao cha Bunge la bajeti kuanza, jambo ambalo ni ukiukwaji wa Kanuni za Kudumu za Bunge.


  Kwa mujibu waKKwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Kanuni za Kudumuza Bunge (Toleo la mwaka 2007), wabunge wanapaswa kupokea vitabu vya makadirio ya bajeti ya serikali angalau siku 21 kabla ya kikao cha Bunge la bajeti kuanza. Pamoja na kwamba kikao cha bajeti kinatarajia kuanza tarehe 12 Juni 2012, hadi kufikia Mei 29, 2012 bado Wabunge walikuwa hawajapokea nyaraka hizi muhimu na haijulikani ni lini watazipokea.

  Hii ni kinyume na kanuni na maazimio mbalimbali yaliyoridhiwa na serikali likiwemo, TAMKO LA DAR ES SALAAM la mwaka 2011 lililotolewa na wananchi na Azaki karibu 100 kutoka nchi mbalimbali duniani na mashirika 12 ya Kimataifa. Tamko hilo linasisitiza uwazi katika bajeti, uwajibikaji na ushirikishwaji kwa kuzitaka Serikali Kuu na Serikali za Mitaa: Kutengeneza na kujadili waziwazi, katika muda muafaka, angalau nyaraka nane muhimu za bajeti: mojawapo ya nyaraka hizo ni makadirio ya bajeti.

  Kutolewa kwa wakati kwa vitabu vya makadirio ya bajeti vya mwaka wa fedha unaofuata kwa Wabunge na umma kwa ujumla, ni hatua muhimu katika kuongeza uwazi, ubora wa bajeti na ufanisi wa ushiriki wa wabunge katika kikao cha kujadili na kuidhinisha bajeti. Hatahivyo, Sikika imebaini kwamba ni kawaida kwa wabunge kupokea vitabu vya bajeti kwa kuchelewa sana, na wakati mwingine huvipata baada ya kikao chabajeti kuanza. Hali hiyo pia inaweza kusababisha wabunge kupitisha bajeti bila kufahamu undani wa kile wanachokijadili au kupitisha bajeti isiyo na tija wala kipaumbele kwa taifa.

  Pamoja na kuchelewa kupatiwa vitabu vya makadirio ya bajeti, Sikika pia imebaini kuwa, wabunge hupatiwa vitabu vya makadirio ya bajeti toleo la I-IV ambavyo kwa kawaida huwasilisha jumla kuu za vifungu bila maelezo ya kina, na huwa hawapatiwi kabisa Vitabu vya Muundo wa Matumizi vya Muda wa Kati vya bajeti (MTEF) kwa kila Wizara, Idara na Mashirika mbalimbali ambavyo ndivyo hubeba maelezo ya bajeti na shughuli zitakazotekelezwa.
  Sikika imekuwa ikipitia tovuti ya Wizara ya Fedha(www.mof.go.tz) na Bunge (www.parliament.go.tz) na kubaini kuwa hadi leo tarehe 29, Mei 2012, vitabu vya bajeti kwa mwaka wa fedha 2012/13 havijawekwa kwenye tovuti hizi mbili. Hii inawanyima Wabunge pamoja na wananchi fursa ya kushiriki kikamilifu katika mjadala wa kuichambua bajeti kabla ya kuidhinishwa na Bunge. Tatizo hili pia lilijidhihirisha mwaka jana (2011), ambapo Wabunge hawakupata vitabu hivyo kwa wakati muafaka. Kwa mwenendo huu, Sikika inauliza, je Wabunge huwa wanapitisha bajeti waliyoisoma, kuitathmini na kujiridhisha kama kweli inakidhi mahitahi ya Watanzania?

  Sikika inatoa rai kwa Serikali kuhakikisha inatoa vitabu vya bajeti vya mwaka wa fedha 2012/13 toleo la I-IV na vitabu vya Muundo wa Matumizi ya Muda wa Kati (MTEF) kwa kila Wizara, Idara na Mashirika Mbalimbali kwa Wabunge kabla ya kuanza kwa kikao cha bajeti. Hii itawapa Wabunge muda wa kufanya uchambuzi wa kina na kushiriki kikamilifu katika mjadala na hatimaye kuidhinisha bajeti yenye manufaa kwa wananchi.

  Serikali pia ihakikishe vitabu hivyo vimewekwa katika tovuti za taasisi husika kabla ya mjadala wa bajeti kuanza bungeni ili kutoa fursa kwa wadau wote kuipitia na kutoa maoni yao kabla ya kupitishwa na Bunge.

  Sikika inaamini kuwa hili linawezekana, na ni vyema Serikali kupitia taasisi husika hasa Wizara ya Fedha pamoja na ofisi ya Bunge kutimiza wajibu na kuhakikisha hazikinzani na taratibu, kanuni na sheria zilizoridhiwa na Serikali kwa kuweka hadharani vitabu vya makadirio ya bajeti mapema na kwa wakati.


  Mr. Irenei Kiria
  Mkurugenzi wa Sikika, P.O. Box 12183 Dar es Salaam,
  Simu: +255 222 666355/57, Nukushi: 2668015, Barua pepe: info@sikika.or.tz, Tovuti: www.sikika.or.tz
   

  Attached Files:

 2. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  lazima magamba yawachomoke mwaka huu.Hapo hakuna kuchomoa.Serikali kuu inapiga udalali kuwa ufisadi na mchwa upo serikali za mitaa na halmashauri wakati serikali kuu ndio balaa sana.Asilimia 27 tu ya bajeti ya serikali mwaka 2011/12 sawa na trilion 3 zilikwenda serikali za mitaa, na 73% zilitumika serikali kuu .Kuna wizara ambazo zinabajeti kubwa lakini hazina uhusiano na serikali za mitaa kama mambo ya ndani,ulinzi,ikulu,viwanda,utumishi na biashara,maliasili,sheria nk.Uchambuzi ufanyike kitakwimu ili kubaini serikali za mitaa perse kunako maendeleo ya wananchi wanapata asilimia ngapi oc+development katika bajeti.Na ndio maana fedha kwenye mawizara zinapatikana za kufisadi na muda mwingi watumishi wanazunguka nje za nchi.
   
 3. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Taarifa hii imenifungua macho. Waoemu mmeshikwa pabaya!
   
Loading...