Vikao visivyoisha maofisini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vikao visivyoisha maofisini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Quemu, Mar 18, 2010.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hizi ofisi zetu zina vikao sijapata ona. Yaani kila ofisi ukijaribu kuweka appointment kumwona mtu fulani, utasikia yupo kwenye kikao tangia asubuhi. Ukisema uje kumwona kesho, utasikia kuwa atakuwa kwenye kikao pia…na keshokutwa….na mtondogoo…wiki mzima.

  Ni hili sio suala la ofisi moja tu. Ukijaribu kukutana na wahusika wako katika ofisi tano tofauti kwa siku, basi nakuhakikishia kuwa wanne watakuwa/utaambiwa kuwa wako kwenye vikao.

  Swali la kujiuliza ni je watanzania wanafanya Kazi saa ngapi, ikiwa kama wanatumia muda wao mwingi kwenye vikao? Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa kila jumatatu na jumatano huwa wanavikao karibu siku mzima. Saa 3 asubuhi wanakikao mpka saa 6 mchana. Wanatoka wanaenda lunch, halafu wana kikao kingine kunanzia saa 8 mpaka saa 10 jioni. Baada ya hapo wanazugazuga kwa lisaa hivi, halafu hao wanachumpa. Siku imeisha. Sasa ukiangalia utaona kuwa, kati ya masaa 40 ya kazi ya wiki mzima, ndugu zetu hawa wanapoteza masaa 16 ya jumatatu na jumatano kwenye vikao. Ina maana wanabakiwa na masaa 24 tu. Na ukitoa muda wa kusoma magazeti, kupiga umbeya, kwenda kununua vocha za simu, kutembelewa na marafiki makazini, n.k… basi utaona kuwa hata hayo masaa 24 yaliyobaki yanautata kwenye kupiga mzigo.

  Nikijaribu kuchambua pengine sababu inayofanya vikao vipewe kipaumbele maofisini, nitakuja na yafuatavyo (hamna mtiririko maalum):

  Maamuzi ya pamoja (jumla)
  Huu mlolongo wa vikao visivyoisha unaweza kuashiria kuwa watanzani ni waoga kufanya maamuzi wenyewe (Individual Decision Making). Badala yake tunapendelea kufanya maamuzi ya pamoja (Collective Decision Making). Kwa nini tunapenda maamuzi ya pamoja? Kwa sababu iwapo mambo yatakwenda tofauti na mategemeo, basi hakuna wa kubeba mzigo wa lawama. Kisingizio kitakuwa ni “si tulijadiliana na kufanya maamuzi wote pamoja.” Hatupendi/tunaogopa ku-take responsibilities.

  Sitting Allowances
  Hili linajulikana kwa upana zaidi. Limeshajadiliwa kwa mapana zaidi katika mada mbalimbali.

  Kuna dada mmoja anafanya kazi kwenye NGO moja hivi ya wazungu inayoshughulika na ishu za uzazi wa mpango na utokomezaji wa magonjwa ya muda mrefu (malaria & co.) katika nchi za duni ya tatu. Sasa siku moja waliandaa kongamano la kujadili jinsi ya kutokomeza/kupunguza magonjwa hayo. Basi wakatuma mialiko kwa wizara ya afya, mahospitalini, na wahusika wa jiji. Unajua nini? Waalikwa wote walitaka wapewe sitting allowances kwenye kongamano linalohusu shughuli ambazo ni sehemu ya kazi zao. Wazungu wakasema “get the f*@$ outta here.”

  Tu wavivu
  Vikao hivi vinaweza pia kuashiria kuwa sisi ni wavivu, tusiopenda kuchapa kazi. Badala yake tupendelea kukusanyika na kupiga soga huku tukisingizia kuwa ni tunajadiliana mambo muhimu ya kiofisi. Unaweza kukuta humo ndani kwenye conference room muda mwingi unatumiwa kwa mabishano na majigambo baina ya wapenzi wa Manchester United, Arsenal na Chelsea, wakati wapenzi wa Liverpool wakigwaya kimya. Au pengine muda mwingi utatumiwa kumzungumzia migogoro ya kisiasa, vituko vya fataki, mambo ya EATV na Ze Comedy yao mpya, na bar zinazopika kitimoto kinono zaidi.

  Yaani iliradi siku inaisha bila kufungua faili lolote lile.

  Hatupendi Ugeni (wa kiofisi)
  Je tunavyoambiwa kuwa fulani yuko kwenye kikao ni kweli? Au pengine huyo fulani amehamua kujifungia ofisini (hope anachapa kazi) na kumwambia administrative assistant wake kuwa watu wote (isipokuwa x, y, na z) wajao kumuona waambie kuwa yuko kikaoni? sidhani kama jibu la swali hili laweza kuaptikana.

  Oh well, sababu zinaweza kuwa nyingi, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa wingi wa vikao hivi hausaidii ufaninisi wa uchapa kazi kama managements zinavyotaka kuamini. Ni upotezaji wa muda, ambao matokeo yake ni ushindwaji wa ufikiaji wa malengo na maazimio.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hama ofisi..........
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kusema kweli tunatatizo kubwa hasa kwa viongozi wanaopewa vijiofisi vwa umma, utakuta baadhi ya ofisi eti wana management meeting kila juma tatu lakini wanajadili nini basi ni kuchukua allowance tu hakuna lingine.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Nadhani hivyo vikao ndo kazi zenyewe. Hao ndo wafanya maamuzi kisha wanawapelekea watekelezaji. Tatizo liko wapi?
   
 5. senator

  senator JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Nimependa hiyo sehemu..Unajua serikalini mishahara ni midogo ukilinganisha na mashirika binafsi/umma na hata hizo NGO ..asilimia kubwa ya watumishi wa serikali wanategemea posho za kwenye vikao, makongomano etc hapo ndo wanapotokea kujazia vipato vyao..Binafsi nimeshashuhudia sana haya mambo ingawa ni sehemu ya kazi yao.Pale BoT kuna majina ya vikao yanaendana na posho..utasikia mtu anasema leo kuna 105 meeting! ukiulizia nini kumbe hapo wanadaka laki moja na tano kama posho ya kikao cha ndani ya ofisi..Hayo ndo maisha ya Bongo...na ndo Bongo tambarare hiyo
   
 6. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,356
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Uvivu mwingi tu.....
  Akili za ubunifu hakuna....
  Utekelezaji baada ya maamuzi ni sifuri....
  Meeengi tu hata hayaelezeki,ofisi zingine zimekufa kisa vikao,maana vikao vinakula sana bajeti...
  Aibu!!!
   
 7. Mama Nim

  Mama Nim Senior Member

  #7
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kusema kweli watanzania tunapenda vikao. Nakubaliana na wewe kwamba tunaogopa kufanya individual decisions bali tunategemea watu wengine kwani tunaogopa lawama. Kitu kingine nilichonotice ni kwamba mabos wengi wanapenda kuitisha vikao au kuhudhuria vikao ili waonekane ni wachapa kazi lakini mwisho wa siku tunamsaidia yeye kufanya kazi zake coz yeye he simply writes the ideas you shared halafu anaziandika kama his own ideas. Mimi huwa naavoid vikao coz you spend muda mrefu wakati kazi zako zimesimama kumsaidia mwingine afanye zake wakati yeye will never assist you in doing your job.
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  vikao ndo safi maana ndo vinavotuweka mjini hapa .....vikao vidumu
   
Loading...