Vijue vitongoji vya Dar es Salaam vinavyotawaliwa na haya makabila makubwa

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,521
21,997
habari humu!
Jiji la dare s salaam linajumuisha makabila ya watu mbali mbali kutoka kila kona ya Tanzania na nje ya Tanzania;

Lakini ukifanya utafti mdogo utagundua makabila yafuatayo ndiyo yaliyo uteka mji kutokana na kila kabila kutawala au kuwa maarufu katika eneo lake jijini dare s salaam;

1. WAKURYA NA WAJITA; Hili kabila limetawala sana maeneo ya Kitunda,kivule, ukonga na gongolamboto, hawa watu ni maalufu sana kwa biashara ya mayai. Ukitembelea maeneo haya unaweza fikiri umeingia mkoa wa mara maana kiila kitu cha kikabila utapata.wana baisikeli ndefu na niwabishi barabarani ajabu.

2. WASUKUMA NA WANYAMWEZI; H ili kabila linapatikana sana maeneo ya kigamboni hususani Kibada,geza,dege na Mbutu, watu hawa ni maarufu sana kwa kulima na kuuza viazi,pia wanafuga ng’ombe wana nguvu sana na niwapole sana, ila ushirikina usiulize, ukienda eneo hilo utadhani umeingia mkoa wa Shinyanga, wanashangaa hadi gari likipita.

3. WACHAGA NA WAPARE; hawa watu wanapatikana sana kimara, mbezi zote na maeneo ya ubungo, Maeneo haya katika nyumba 10, basi saba ni wachaga, na athili yao ya kufuga ng’ombe wa maziwa, maeneo haya kitimoto kama kawaida, hadi kuna mtaa unaitwa ROMBO.Ingawa watu hawa kwa upande wa Tegeta kuna mchanganyiko na wahaya

4. WAMAKONDE NA WADENGELEKO; Haya makabila buana mbagala, yaani mbagala wapo wa kumwaga nazani ni kwasabu ya stend ya mtwara ipo mbagala.ingawa kwa sasa mji wa mbagala unapanuka kwa kasi wanaonekana kumezwa na mwingiliano; Ila sifa kuu ni wabishi balaa halafu hata kama hawajui kitu.

5. WAZARAMO; Hawa watu buana, kwa mbagala kiasi wapo, lakini utawapata kwa wingi pembezoni hususani mkuranga,kisemvule na maeneo ya Kimbiji, hawapendi shida , nyumba zao nyingi ni za nyasi.

Kama unataka kujifunza mila na destuli za makabila hayo, hauhitaji kusafiri hadi mkoani, wewe tembelea maeneo hayo utaamini ninachokwambia. Kama kuna kabila lolote kubwa tofauti na haya jijini dare s salaam tujuze hapa mtaa na sifa zao.
masai.jpg
wasukuma.jpg
 
Utafiti wako una ka ukweli japo haujajitosheleza.
Kitunda na kivule ni eneo dogo na ambalo halijajengeka kivile so wakazi wake nao sio wengi kivile, japo ni kweli wakurya na wajita wame dominate lakini sio kwa kiwango cha kuzidi makabila mengine.
Ukweli ni kwamba mchaga yuko kila kona ya Dar
 
Utafiti wako una ka ukweli japo haujajitosheleza.
Kitunda na kivule ni eneo dogo na ambalo halijajengeka kivile so wakazi wake nao sio wengi kivile, japo ni kweli wakurya na wajita wame dominate lakini sio kwa kiwango cha kuzidi makabila mengine.
Ukweli ni kwamba mchaga yuko kila kona ya Dar

Mchagga kama Mchina kila kona ya Tanzania yupo!!
 
munadhani kabila gani alipo kila eneo dar, kuna makabila yamezoea kujipendelea yaani ndo asili yao kila mahali wanaona wapo wao. Mtoa mada kaeleza vizuri kuhusu baadhi ya makabila yame- dominant baadhi ya maeneo. wachaga wako mbezi ndo Barabara ya kwenda kwao, wamakonde wako mbagala ndo njia ya kuelekea kwao hata mabasi yao machache sana yanayoazia ubungo au kuishia safari ubungo.
 
Back
Top Bottom