vijiviswali kidogo wadau!!!

vijiviswali kidogo wadau!!!

PAPAKINYI - SJUT 2013

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2017
Posts
367
Reaction score
251
juzi kati hapa kulipita mambo mawili (2); moja ilikuwa ni ALBADIR ambayo, nasikia, ilikuwa ni ya nchi nzima (kusomwa). pili ilikuwa ni kuvunjwa kwa chungu huko upareni (kilimanjaro). matukio yote haya yaliasisiwa na chama fulani ili yaende kuathiri (kudhuru) chama kingine fulani hivi ambacho kina madaraka nasikia. kelele zilikuwa nyingi sana na mioyo myepesi kujazwa hofu kuwa kuna jambo kubwa litatokea kwa walengwa!

nasikia kabla ya albadir hiyo na uvunjaji wa chungu huo wanachama na madiwani walikuwa wengi sana kwa upande waasisi wa albadir.....

hapa juzi tu tena umepita uchaguzi, kutokana na albadir, watu walitegemea anguko kubwa la chama tawala katika hizo kata......cha ajabu wale waliosoma albadir na kuvunja vyungu ndo wamepigika vibaya katika uchaguzi huo kwani nasikia wameambulia kiti kimoja (1) tu kati ya arobaini na tatu (43). kutokana na hilo, nina vijiviswali vifuatavyo;
  • albadir ilisomwa vibaya na hivyo kumgeukia msomaji, au?
  • hakukuwa na wasomaji wazuri kama wale wa kilwa, au?
  • mungu hasikilizi wanafiki (wanasiasa), au?
  • funzo gani tunaweza kulipata baada ya tukio hili la kushindwa kwa albadir na vyungu?
  • kinachofuata ni nini baada ya albadir kushindwa?
 
Back
Top Bottom