Vijiji 87 kongwa kupata umeme

Vijiji 87 kongwa kupata umeme

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
1078230


WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema hadi ku ka Julai mwaka huu, vijiji 87 katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma vitakuwa vimeunganishwa na umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini, Awamu ya Tatu (REA III).

Dk Kalemani aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngonga wilayani Kongwa mwishoni mwa wiki, wakati wa sherehe za kuwasha umeme katika kijiji hiyo. Dk Kalemani alisema wakandarasi waliopewa kazi ya kupeleka umeme kwenye vijiji hivyo watafungua osi eneo la mradi kwa ajili ya kuwezesha ulipaji wa ada ya huduma ya kuunganisha umeme.

“Wenye nyumba mnaweza kuanza kulipa gharama za kuunganishiwa umeme. Wananchi mnatakiwa kufahamu kuwa gharama za kuunganisha umeme ni Sh 27,000 tu.” Dk Kalemani ambaye aliongozana na Mbunge wa Kongwa (CCM) na Spika wa Bunge, Job Ndugai ambao walifanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo wa REA III aliwasha umeme kwa mara ya kwanza kwa vijiji ambavyo tayari vimekishiwa huduma ya nishati hiyo.

Pia Dk Kalemani alitumia fursa hiyo kumwagiza mkandarasi, A2Z Infra Engineering Limited ambaye amepewa kazi ya kutekeleza miradi ya kupeleka umeme katika vijiji vya Chamwino na Kongwa kurejea katika Kijiji cha Nyerere kutokana na kuwapo kwa malalamiko ya baadhi ya wananchi kukosa fursa ya kuunganishiwa umeme.

“Nimepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao wamekosa nafasi ya kuunganishwa huduma ya umeme katika Kijiji cha Nyerere baada ya mkandarasi kufunga osi kabla ya wao kupata huduma hiyo. Hivyo namuagiza kurejea tena kwenye kijiji cha Nyerere na ahakikishe nyumba zinaunganishwa na huduma ya umeme,” alisema.

Dk Kalemani alitoa rai kwa wajumbe wa nyumba kumi kumi kuhakikisha wanahamasisha wananchi wa maeneo yao ili waunganishwe na huduma ya umeme na kuwa viongozi wa umma wana wajibu wa kuhakikisha wananchi wanaunganishwa na huduma hiyo hasa pindi miundombinu inapopelekwa kwa mara ya kwanza.

Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai alitoa shukrani zake kwa serikali ya awamu ya tano kwa juhudi za kuhakikisha inapeleka huduma ya umeme vijijini, na kuongeza kuwa huduma hiyo itachangia kazi ya ukuaji wa maendeleo ya kijamii na uchumi. Ndugai alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa kijiji cha Ngonga kutumia huduma ya umeme kwa kuanzisha shughuli au biashara za kuwaongezea kipato.

Kwa upande wa mwanakijiji cha Ngonga, Anna Nyalupala ambaye ni miongoni mwa wananchi ambao nyumba zao zimeunganishwa na umeme alionesha furaha yake kwa kuunganishwa na huduma hiyo ambayo alisema itasaidia kuinua kiwango cha ufaulu kwa watoto kijijini hapo. “Kwa sasa watoto wetu wataweza kurejea na kujisomea masomo yao nyakati za usiku. Kabla ya kupata huduma ya nishati ya umeme walilazimika kusoma hadi jioni kabla giza haijaingia,” alisema.
 
Back
Top Bottom