Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Vijana nchini Tanzania hususani waliopo vyuoni wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kudumisha utulivu, amani na kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Wito huo umetolewa na Mdau wa Maendeleo na mwanasiasa wa mkoani Iringa Shalom Robert wakati akizungumza na Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la chuo Kikuu cha Iringa ulifanyika katika ukumbi wa CCM kata ya Kihesa.
Shalom ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo alisema wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu kuna kuwepo na vitendo mbalimbali viovu ikiwemo rushwa hivyo ndio wakati wa vijana kupambana navyo na kuviepuka na kudumisha utulivu na amani.
“Naombeni twendeni tukaepuke rushwa kwasababu Kuna mambo kadha wa kadha huwa yanatokea Katika kipindi hiki Vijana twendeni tukapinge hayo mambo maovu lakini twendeni tukamsikilize yule mwenye sera ambaye yupo tayari kutuongoza” alisema