Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,607
Takwimu zinaonyesha kuwa vijana na watoto nchini ndiyo wanaoongoza kupata maambukizo ya Virusi vya Ukimwi (VVU) duniani.
Takwimu za hivi karibuni za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya Ukimwi (UNAIDS) zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya maambukizi mapya ya VVU duniani yanatokana na vijana kuanzia miaka 15 hadi 24.
Meneja mawasiliano na uraghibishi kutoka taasisi ya Elizabeth Glasser inayopambana na ukimwi kwa watoto (Egpaf) Mkama Mwijarubi, alisema hayo jana akiwa katika klabu za watoto waishio na VVU Hospitali ya Kibosho na KCMC zilizopo Mkoani Kilimanjaro.
Mwijarubi alisema vijana wengi wameathirika kwa sababu ya kutokuwa na tahadhari yoyote na hivyo kuendelea kuambukizana wenyewe kwa wenyewe na kuchangia kuendelea kuwapo kwa maambukizo mapya.
Alisema idadi kubwa ya watoto wameambukizwa na wazazi wao tangu wakiwa tumboni na hivyo wanapozaliwa wanakuwa tayari wameathirika.
“Kutokana na changamoto hiyo taasisi hiyo ilifikia hatua ya kuwekeza kuwaangalia watoto na vijana kuanzia umri wa 0 hadi miaka 14 ambapo kijana akifikisha umri wa miaka 17 humwacha ajihudumie mwenyewe,” alisema.
Mkurugenzi Mkazi wa Egpaf, Jeroen Van’t Pad Bosch alisema taasisi hiyo ilianza kufanya kazi nchini tangu mwaka 2003 lengo likiwa ni kupambana na VVU kwa watoto.
Mwananchi