Vijana wa Kitanzania tulipoteza wapi Uaminifu?

Vijana wa Kitanzania tulipoteza wapi Uaminifu?

black abdu

Senior Member
Joined
Dec 2, 2022
Posts
157
Reaction score
214
Juzi kuna mshakaji wangu ameomba nimuazime kiasi kidogo cha fedha kwa ahadi ya kurudisha siku inayofuata...lakini hadi sasa amepiga kimya... kabla ya huyu kuna mwingine aliomba nimuazime pia, mshahara wake ukitoka angenirejeshea, nae hadi leo kimya.

Nawaza labda mambo yao hayajakaa sawa, lakini hata text tu ya kusema "samahani nitachelewa kidogo na amana yetu"?!

Haikuanzia kwa hawa wawili, huko nyuma nilimuazima mtu pesa ku-boost mtaji wake, lakini hadi leo amebaki na 5k baada ya kulipa kwa mbinde hadi ilifikia siku nilichukua bidhaa yake nikamwambia akate kwenye salio la deni. Mwengine nimemsamehe 30k, aliazima pesa ndefu kiasi kuwa anashida ya upesi lkn hadi nilitengeneza uongo kuwa pesa niliyompa niliazima kwa mtu na mwenyewe anataka kuja kuchukua vitu vya ndani, ndio akaanza kulipa kidogo kidogo na uongo mwingi.

Siku moja mshikaji kanieleza fikra yake ya biashara nikajitoa kiherehere kumkopesha pesa ya mtaji, tena niliazima kwa mtu lakini sikuona senti tano na ikabidi lile deni nilikipe mwenyewe.

Kinachofuata ni kuwa nitafunga milango ya kusaidiana, yaani mtu akija na shida zake labda nimpe kama mchango na si mkopo, na hapo itategemea niwe na pesa ambayo haitaacha "gepu" endapo nitaitoa.

Siku hizi ndio ule usemi ukimkopesha rafiki yako jiandae kupoteza pesa na kumpoteza rafiki, ila rafiki wa kweli huwezi kumpoteza kama ni mwaminifu na kama si mwaminifu hafai kuwa rafiki!
 
Hao uliokutana nao ndio labda sio waaminifu ngoja na mm nikupe mifano ya waaminifu

Wa kwanza ni mdada alikua anaanza chuo alipungukiwa hela kama 250K akanieleza nikamlipia vzr baada ya kusaini hela ya meals and accomodations akanirudishia on time kabla ya mda alioniahidi!

Wa pili; Boss mzenji hua anantumia hela nafanya manunuzi then napeleka Azam namtumia kama mara mbili nlinunua kwa hela yangu nikamtumia mzigo aliuza ulivoisha akantumia hela yangu 850k

Wa tatu; Mwalimu wa sec nlikotoka aliniomba gunia moja la mahindi alipie chakula kwa vijana wake nkampa mwisho wa mwezi akanipa hela yangu.

Pia nshakutana na watu ambao sio waaminifu lkn sio katika kiasi unachotaka kutuaminisha ndugu mwandishi
 
Ilitakiwa isomeke " Marafiki zangu wamepoteza wapi uaminifu" na sio kila kijana wa kitanzania.
 
Back
Top Bottom