Mchimwachimego
JF-Expert Member
- Jun 15, 2020
- 358
- 271
Kiumri mimi siwezi kujiita kijana ila nimepitia huko katika nchi yetu hii Tanzania nguvu kazi kubwa ni vijana wasomi na wasio wasomi hawa wote hulka zao nazifananisha na fisi msituni, maisha yake yote fisi msituni utumia nguvu nyingi katika kunyang'anya mawindo ya wanyama wengine, kuokota mizoga, kuwinda wanyama wagonjwa na ndama.
Fisi hajui mbinu za kuwinda, ratiba yake ya kesho itajulikana kesho yeye hawezi kujitafutia kwa akili zake na maarifa yake yeye utegemea wenzake wafanye kazi ili ale makombo au apole kwa nguvu.
Hivyo hivyo ndivyo vijana wengi wa Kitanzania walivyo na tabia za fisi ukiwakuta katika maongezi na mipango wanayoizungumzia unaweza kusema hapa tuna wasomi lakini vitendo ni bure kabisa, mtu amesomea teaching, mifugo, kilimo, biashara, mipango miji, fundi mitambo, ujenzi nk: lakini ukimwambia afanye alichikisomea hawezi kazi yao ni kufuga vitambi na kulalamikia mishahara.
Wapo wengine huku mitaani wanaamini kuwa ukiwa na degree basi wewe kazi yoyote ya mikono haikuhusu na si hadhi yako, nawaomba vijana mubadilike elimu ni kuongeza maarifa tu ni lazima muvifikilishe vichwa vyenu kugungundua na kubuni fulsa mpya na vitu vipya vitakavyowaongezea ubunifu zaidi, kwenye ulimwengu wa leo ukianzisha kitu kipya kitakupa faida sana kuliko kuiga cha mwingine.
Asanteni.