Vijana wa internship na ajira yangu

Godwin peter

JF-Expert Member
May 12, 2019
360
605
Habarini humu wadau,

Naombeni muongozo au kama nyie mshawahi kukutana na hali kama hizi mnazikabili vipi.

Kiufupi ni kwamba nimeajiriwa kwenye company moja hivi, sasa nipo kwenye matazamio ya miezi mitatu, sasa katika ile company kuna vijana wawili same age kama yangu waliingia kama intern hawa vijana wana unaa sana na kazi.

Yaani naona ajira yangu ikipotea kwasababu wanajituma sana hata kutoka ofisini wao wanakuwa wa mwisho na kuingia wao ndio wa kwanza kiasi kwamba hadi wakuu hapo wataona ni bora wawachukue wao waniache mimi.

Je, ushawahi kukumbana na hii kadhia ofisini kwako na je vipi uliweza kui-handle hii situation.

Note: Mtaani pagumu
 


Je unatimiza majukumu 100%? kama ndio basi usiwe na wasiwasi

Ningekua mimi ndo naajiri ningeangalia production (ufanisi) wako na sio kuwahi na kuchelewa kutoka kazini.

Na kama sio riziki yako sio tu,

Pray Trust and wait.
 
Pole sana ila hii kitu sasa hivi mashirika mengi wanaita watu kwenye ajira halafu wanasema ni 'interns' au 'volunteers 'ni aina ya unyonyaji wa ajira za vijana.

Serikali imeweka sheria kali ya pension kuwa 'temporary staff' walipiwe NSSF inapelekea mashirika mengi hasa yasiyo ya kiserekali sasa kuwaajiri watu kwa mtindo wa interns na volunteers huku wakiwalipa pesa kidogo.

Anyway nahisi niko nje ya mada ila Serikali iliangalie hili janga la watoto wetu kutumikishwa kwa njia hiyo wakiambiwa wanajifunza kumbe sio kwani utakuta mtu amesoma HR sasa anakimbizana na data za Covid huko mtaani.
 
Nchi yetu mtu akifanya kazi kwa bidii anaitwa "Mnaa".

Hiyo ndio sababu hatuendelei. Ndio maana ukienda ofisi za Serikali huko, hadi secretary anajiona Mungu mtu. Watu wanafanya kazi kwa mazoea tu.

Kama mimi ndio muajiri, basi ningewaajiri hao vijana. Ni boss gani ambae hataki mfanyakazi mwenye bidii?
 
Nchi yetu mtu akifanya kazi kwa bidii anaitwa "Mnaa".

Hiyo ndio sababu hatuendelei. Ndio maana ukienda ofisi za serikali huko, hadi secretary anajiona mungu mtu. Watu wanafanya kazi kwa mazoea tu.

Kama mimi ndio muajiri, basi ningewaajiri hao vijana. Ni boss gani ambae hataki mfanyakazi mwenye bidii?

Hao wanaa kweli, wana bidii mwanzoni because they want the job... wakiajiriwa wataacha hiyo bidiii trust me

Mtoa mada wewe endelea kuwa consistent fanya majukumu yako, ongeza value kazini achana na hivyo vihere here, hao ndio waliokuwa wanauliza mwalm wa mathe mbona hatuachii homework.
 
Back
Top Bottom