Vijana tusishikiwe akili

Vijana tusishikiwe akili

Aisha Iddi

Hakika wewe ni lofa na mpumbavu! Tunataka tupate mtu atakayebadili mfumo uliopo na tupate katiba yenye kuwawajibisha viongozi ndio utaona kua ahadi zote zinatekelezeka! Kwa katiba mbovu iliyopo na hata inayopendekezwa hakuna sehemu ya kuwawajibisha watoa ahadi hewa.Kwa ufinyu wako wa mawazo unashindwa hata kufikiria kua kinachotusumbua ni mfumo mbovu uliopo.
 
Last edited by a moderator:
Uloi nga mâché68;14060267 said:
Mabadilikho yanaletwaje na walioshindwa Uchaguzi CCM? Tumieni japo moja ya mia ya akili zenu!
Hakuna anayeweza kufikiri kama wewe! Wengi akili zao zimeshikiliwa na Form four Mbowe!
 
Asante ndugu kwa msaada wako,maana kwa sasa watu akilini kinachozunguka ni ushabiki na siyo,tafakuri kwamba kwanini awe huyu na asiwe yule,kisingizio ati tumechoka ugali twataka mihogo,mihogo mingine ni mihogo mwitu ina sumu bora kuendelea na ugali ukiwa hujala sumu

Pumbav.u
 
ata akihaidi mabomba yatatoa maziwa sisi tutamchagua tu
 
Haja yangu CCM iondoshwe tu baasii,hapo tutaanza upya
 
Sisi Hatutaki Ccm Habari Za Ajira Tutajulia Huko Lakini Ccm Iwe Haipo
 
Upo mchezo mchafu wa baadhi ya wanasiasa kuwadanganya watu wenye hali za chini na wanaotafuta ajira kuwa watawapatia ajira na watawaboreshea maisha yao.

Jambo baya kwenye mchezo huo ni kuwapa watu matumaini makubwa yaliyo nje ya uwezo wa nchi yetu hata kama Obama akiletwa awe Rais wetu kwa miaka kumi hawezi kutekeleza ahadi hizo

Hivi kweli mtu anayetaka Urais aseme bado siku 50 mwenye ng'ombe wawili atakua na ng'ombe wanne? ni kweli baada ya siku 50 mwenye kibajaji atakuwa na gari?

Kutokana na ugumu wa maisha na ukossefu wa ajira watu hawa wanakubali kwa shangwe na kuunga mkono bila kupima uhalisia wa mambo ulivyo.

Ni kweli kuna tatizo la ajira lakini ukweli ni kwamba hilo ni tatizo la dunia nzima, kila nchi inajitahidi kutatua tatizo hilo kadiri ya uwezo wa nchi hiyo, lakini siyo kudanganya watu kua bado siku 50 kila asiye na ajira atapata ajira.

Mtatumika kuwapigia debe wagombea hao, mtaandamana, mtavunjwa miguu lakini wakipata fursa ya kuingia ikulu watawasahau na kubadilisha kauli zao kwakua waliahidi vitu visivyowezekana.

Hivi umeshawahi kuona au kusikia nchi ambayo watu wake wote wana ajira? katika dunia hii ni rais gani aliweza kuwatoa watu wote wenye pikipiki hadi kumiliki magari tena ndani ya muda mfupi?

Umasikini wenu ni mtaji wao wa kisiasa, wanasema kwa ncha za ndimi zao lakini ndani ya nyoyo zao hawamaanishi wakinenacho. kuweni watulivu kisha mupembue sera kwa kuangalia uhalisia na utekelezaji wake. Najivunia kusema kuwa Magufuli ndiye mgombea bora mwenye sera zinazotekelezeka.

Nawatakia kila la heri kwenye safari hii ya kuelekea October 25, safari iliyobeba maisha yetu ya miaka mitano kama si kumi.

Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Ukitaka kuwa kichaa jiajiri kwa kufanya kazi au biashara inayotegemea umeme hapa tanzania.Ukweli au Uongo?
Jukumu la kuhakikisha umeme wa uhakika ktk nchi ni la nani?
 
wanadanganywa watapewa ajira bwelele wakiwasaidia kwenda ikulu, wanaambiwa pesa zitakua nje nje tu wakiwapetisha wao kwenye uchaguzi, wanawadanganya hawatokuwa boda boda tena endapo watawachagua kwenda ikulu kumbe hawajui mbinu za wanasiasa uchwara wa bongo. Huu ni uongo wa asubuhi kweupe kabisa, pesa zitaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za kiuchumi ili kuzuia mfumuko wa bei, siyo kumwaga pesa hovyo kisa mumewachagua. Ajira zitatolewa kwa uwezo wa serikali kuwalipa watumishi na uwezo wa wawekezaji kuendesha uchumi wao. Hata ukienda uingereza kuna shida kubwa ya ajira, hakuna nchi inayoweza kuotoa ajira kwa watu wake wote, na huwezi kuiacha kazi yako ya boda boda baada ya kupita Rais fulani, tunachotaka ni unafuu wa maisha tu
 
Asante ndugu kwa msaada wako,maana kwa sasa watu akilini kinachozunguka ni ushabiki na siyo,tafakuri kwamba kwanini awe huyu na asiwe yule,kisingizio ati tumechoka ugali twataka mihogo,mihogo mingine ni mihogo mwitu ina sumu bora kuendelea na ugali ukiwa hujala sumu
Kama ni huo unaouita ugali, tushaula kwa zaidi ya miaka 50 kwa hiyo hivi sasa ushatukinai ile mbaya.

Ni lazima kabisa mwaka huu tubadilishe diet, hata kama ikibidi tutoke kwenye ugali wa sembe, hivi sasa tutaanza kula ugali wa mihogo.

Ukitaka kujua umuhimu wa kubadilisha diet, hata yule Dr Mihogo ameamua kuikimbia diet ya mihogo ya hapa nyumbani na hivi sasa kakimbilia Marekani ili abadilishe diet ya mihogo na huko 'majuu' hivi sasa anajichana mapiza!

Kwa hiyo mwaka huu hakuna namna nyingine bali tu MABADILIKO ni LOWASSA na LOWASSA ni MABADILIKO

Hata kama atakuwa anatembelea wheel chair, bado tutampeleka Ikulu Edo wetu ndani ya wheel chair yake hivyo hivyo!
 
Ndio kampeni zenu za vitisho nyie wapumbavu. sisi tumekwisha amua, tunataka uchaguzi huru la sivyo tutaandamana pasipo kikomo mtuue. Kwanza tanzania haina amani ni kuvumilia tu

nenda kongo ndo utajua tanzania kuna amani au maigizo. usisahau kutembelea kaskazini mwa uganda na eneo kati ya ethiopa na kenya.

sisi tulikuwa na changamoto za viongozi wetu kuwa na tamaa na hizi kwishnei kipindi cha magufuli. lakini hapa amani ipo. kama unaona haipo hujachunguza majirani zetu wanaishije. tembea uone.

tanzania hii unatembea kaskazini mpaka kusini, magharibi mpaka mashariki popote ufikapo ukiwathibitishia wewe ni mtanzania unapokewa. kwa wengi wa majirani zetu hali haiko hivo

acheni uongo
 
hapa tunashuhudia kwa uzuri kabisa mtu aliyeenda shule halafu hajaelimika anakuwaje.

anakwambia ccm kuna ufisadi wa escrow na nk. sawa. lakini anaishia hapohapo. haendi mbali kutaka kuona umekujaje. nani aliuleta. huyo rais anayekuja ana historia gani / rekodi gani kwenye hii changamoto kubwa ya ufisadi. kazi ya urais si ya kulala kitandani, hivyo, je, huyo ajaye ataweza mudu mikiki mikiki ya kila siku? hilo kundi linalokuja lina uwezo gani? lina mipango ipi? au kila mmoja na mipango yake? au ni kundi kubwa ambalo lina vikundi vingi na kila kikundi kina mipango yake?

mambo ya kuya chunguza ni mengi na yote ya muhimu

lakini mwisho wa siku jawabu utakalo lipata ni kuwa ccm chini ya magufuli ndio chaguo bora. ukiwa mtu makini huwezi mlinganisha magufuli na lowasa. saizi ya magufuli alikuwa dr slaa. japokuwa chama chake kingemuangusha
 
Kwani tatizo ni nini? Ccm mnashangaza kwani wanaongoza nchi ni chama gani? Kama watu wamewachoka mnataka kuwalazimisha kwa nini halafu kila mtu ana haki ya kuchagua anayemtaka ndio democrasia
 
Back
Top Bottom