Vijana tusishikiwe akili

Vijana tusishikiwe akili

Mariswaga

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2015
Posts
201
Reaction score
2
Upo mchezo mchafu wa baadhi ya wanasiasa kuwadanganya watu wenye hali za chini na wanaotafuta ajira kuwa watawapatia ajira na watawaboreshea maisha yao.

Jambo baya kwenye mchezo huo ni kuwapa watu matumaini makubwa yaliyo nje ya uwezo wa nchi yetu hata kama Obama akiletwa awe Rais wetu kwa miaka kumi hawezi kutekeleza ahadi hizo

Hivi kweli mtu anayetaka Urais aseme bado siku 50 mwenye ng'ombe wawili atakua na ng'ombe wanne? ni kweli baada ya siku 50 mwenye kibajaji atakuwa na gari?

Kutokana na ugumu wa maisha na ukossefu wa ajira watu hawa wanakubali kwa shangwe na kuunga mkono bila kupima uhalisia wa mambo ulivyo.

Ni kweli kuna tatizo la ajira lakini ukweli ni kwamba hilo ni tatizo la dunia nzima, kila nchi inajitahidi kutatua tatizo hilo kadiri ya uwezo wa nchi hiyo, lakini siyo kudanganya watu kua bado siku 50 kila asiye na ajira atapata ajira.

Mtatumika kuwapigia debe wagombea hao, mtaandamana, mtavunjwa miguu lakini wakipata fursa ya kuingia ikulu watawasahau na kubadilisha kauli zao kwakua waliahidi vitu visivyowezekana.

Hivi umeshawahi kuona au kusikia nchi ambayo watu wake wote wana ajira? katika dunia hii ni rais gani aliweza kuwatoa watu wote wenye pikipiki hadi kumiliki magari tena ndani ya muda mfupi?

Umasikini wenu ni mtaji wao wa kisiasa, wanasema kwa ncha za ndimi zao lakini ndani ya nyoyo zao hawamaanishi wakinenacho. kuweni watulivu kisha mupembue sera kwa kuangalia uhalisia na utekelezaji wake. Najivunia kusema kuwa Magufuli ndiye mgombea bora mwenye sera zinazotekelezeka.

Nawatakia kila la heri kwenye safari hii ya kuelekea October 25, safari iliyobeba maisha yetu ya miaka mitano kama si kumi.

Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
 
Kilio changu ni kwamba ccm iondoke madarakani tu baaaaaasi, tujipange upya........ Taifa limedumazwa viongozi wakicheka cheka, tena ccm inapoteza umakini kadiri siku zinavyo songa.
 
Pole sana tunahitajii mabadiliko tuu na sivinginevyoo
 
Hatujashikiwa akili na ndo maana chaguo letu ni lile lile, Lowassa.
Ya Ngoswe mwachie Ngoswe.
 
Aisha Iddi

Kwahiyo Magufuli kadanganya?

Ameahidi ajira kwa vijana na kujenga viwanda kila wilaya ataweza vipi? 50Million kila kijiji na kila kata... Maisha mazuri kwa walimu kama mapadri.... zahanati...hospitali kote nchini... barabara za lami kote nchini... madawati na dawa za kutosha kote nchini hizi ahadi vipi?

Je umejiuliza haya ya mgombea wako au huna ufahamu wa kutosha?

JK aliahidi ajira kwa vijana ziko wapi?
 
Last edited by a moderator:
Aisha Iddi

Ujinga huu tafuta wapuuzi wenzako kama mjadiliane sisi tumesema hapa ni lowassa tu
 
Last edited by a moderator:
Nashindwa hata kukujibu kitaalam,maana naona nitapoteza muda wangu.
Tafuta vitabu vya UCHUMI WA SIASA UJISOMEE UTOE UJINGA
 
Lowasa ndio rais ,ahadi zake zinatekelezeka...ccm walituahidi meli mpya ziwa victoria wameshindwa kutekeleza...Lowasa ameahidi meli mpya ya kisasa,,viva Lowasa
 
Una minyo..o dume wanakusumbua wewe. Pu..mbavu kabisa.
 
Upo mchezo mchafu wa baadhi ya wanasiasa kuwadanganya watu wenye hali za chini na wanaotafuta ajira kuwa watawapatia ajira na watawaboreshea maisha yao.

Jambo baya kwenye mchezo huo ni kuwapa watu matumaini makubwa yaliyo nje ya uwezo wa nchi yetu hata kama Obama akiletwa awe Rais wetu kwa miaka kumi hawezi kutekeleza ahadi hizo

Hivi kweli mtu anayetaka Urais aseme bado siku 50 mwenye ng'ombe wawili atakua na ng'ombe wanne? ni kweli baada ya siku 50 mwenye kibajaji atakuwa na gari?

Kutokana na ugumu wa maisha na ukossefu wa ajira watu hawa wanakubali kwa shangwe na kuunga mkono bila kupima uhalisia wa mambo ulivyo.

Ni kweli kuna tatizo la ajira lakini ukweli ni kwamba hilo ni tatizo la dunia nzima, kila nchi inajitahidi kutatua tatizo hilo kadiri ya uwezo wa nchi hiyo, lakini siyo kudanganya watu kua bado siku 50 kila asiye na ajira atapata ajira.

Mtatumika kuwapigia debe wagombea hao, mtaandamana, mtavunjwa miguu lakini wakipata fursa ya kuingia ikulu watawasahau na kubadilisha kauli zao kwakua waliahidi vitu visivyowezekana.

Hivi umeshawahi kuona au kusikia nchi ambayo watu wake wote wana ajira? katika dunia hii ni rais gani aliweza kuwatoa watu wote wenye pikipiki hadi kumiliki magari tena ndani ya muda mfupi?

Umasikini wenu ni mtaji wao wa kisiasa, wanasema kwa ncha za ndimi zao lakini ndani ya nyoyo zao hawamaanishi wakinenacho. kuweni watulivu kisha mupembue sera kwa kuangalia uhalisia na utekelezaji wake. Najivunia kusema kuwa Magufuli ndiye mgombea bora mwenye sera zinazotekelezeka.

Nawatakia kila la heri kwenye safari hii ya kuelekea October 25, safari iliyobeba maisha yetu ya miaka mitano kama si kumi.

Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania

umetumia mda mwingi kuandika ujinga!!! POLE SANA kwa mawazo mfu.
 
.......mwaka huu ni LUWASSA tu na hatukubali kushikiwa akili zetu na maccm
 
Nahisi ameshaj...in..yea maana alikuwa anatafuta apetite.
 
Asante ndugu kwa msaada wako,maana kwa sasa watu akilini kinachozunguka ni ushabiki na siyo,tafakuri kwamba kwanini awe huyu na asiwe yule,kisingizio ati tumechoka ugali twataka mihogo,mihogo mingine ni mihogo mwitu ina sumu bora kuendelea na ugali ukiwa hujala sumu
 
Ndio kampeni zenu za vitisho nyie wapumbavu. sisi tumekwisha amua, tunataka uchaguzi huru la sivyo tutaandamana pasipo kikomo mtuue. Kwanza tanzania haina amani ni kuvumilia tu

Maneno yako tu yanatosha kujua wewe ni mtu wa aina gani??
 
Ndio kampeni zenu za vitisho nyie wapumbavu. sisi tumekwisha amua, tunataka uchaguzi huru la sivyo tutaandamana pasipo kikomo mtuue. Kwanza tanzania haina amani ni kuvumilia tu

Wapumbavu kinanani said ya cdm
 
Back
Top Bottom