Vijana tushike Dola ya siasa kuanzia Udiwani mpaka Ubunge uchaguzi huu 2020

Street Hustler

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,146
4,194
Habari wajuzi wa Mambo,

Leo nimekuja hapa kisiasa kidogo nia ni kuwakumbusha vijana kuwa sisi ndio wengi na ndio chachu ya maendeleo katika taifa letu lakini sisi ndio wa kwanza kulalamika ilhali sisi ndio wenye nguvu ya kuamua Jambo na likawa.

Binafsi naona huu uchaguzi 2020 unatufaa sisi vijana kujitoa na kwenda kutengeneza Sera nzuri za kuliokoa taifa letu n muda wa kuwaondoa watu wasiostahili kuwawakilisha wanajamii kwanza wanapoteza nguvu ya jamii husika kwa wananchi wao pili wanalifanya taifa lizidi kuwa maskini.

Tujiulize tunashindwa kuwaunganisha vijana wetu pamoja na serikali kutatua changamoto zinazowazunguka, tunashindwa kubuni miradi/huduma za kuwafanya akina mama wapate mazingira mazuri ya nyumban na shughuli ndogondogo binafsi?

Nimeanza kufikiria ipo haja yakuomba uwakilishi katika jamii yangu katika ngazi ya ubunge Sina visenti Wala mahela but I know ninakitu special Cha kuibadili jamii yangu kupitia changamoto zinazowazunguka bila kusumbuana na mipango ya serikali.

Nakusudia kuomba ridhaa hii kupitia Chamà Cha Mapinduzi katika Jimbo Moja hapa Tanzania.

Nakaribisha maoni kuhusu Vijana na siasa za Tanzania hasa katika kubadilisha fikra na ziwe za kufanya kazi na kutatua changamoto karibuni.
 
Una mtazamo hasi sana na hapo ndipo vijana tunakwama. Nia yako si ya kweli ,mtu mwenye nia ya kweli haamini pesa ni kikwazo. Tafuta namna nzuri ya watu kukubali jinsi ulivyo kuliko kuamini mwenye pesa ndio anakubalika.

Badili mtazamo wako juu ya waliotangulia hususani uwezo ,juhudi na maarifa yao katika kulisaidia taifa hili. Kila kilichofanikiwa katika taifa hili ni jitihada za kila mtu licha ya kwamba wengine hawakufanya vizuri lakini mchango wao ni muhimu sana.

Mawazo yangu juu ya sisi vijna

1. Vijana wanahitaji kujifunza sana juu ya uongozi kuliko wao kuwa sehemu ya uongozi. Badala ya kuwaamini vijana katika nafasi kubwa za uongozi na maamuzi ni vema wakaanza kuaminiwa kwa nafasi ndogo

2. Jukumu wa wazee katika kuonya viongozi vijana ni kubwa sana katika jamii zetu hivyo kuna wasiwasi vijana wengi wanapoaminiwa kwa nafasi za juu jukumu hili litapuuzwa.

3. Kuna baadhi ya maamuzi kuyafanya inahitaji maamuzi ya wazee ,vijana wengi wanapoaminiwa maamuzi hayo yatafanyika bila busara na hekima

4. Vijana watakaona siasa ni ajira ndipo tatizo kubwa sana litakapoibuka kwenye taifa letu la kushindwa kufanya kazi au kutegemea siasa.

Ni hayo tu ninayoyaona kwetu sisi vijàna kwenye siasa
 
KARLO MWILAPWA,

Umeongea vyema

1. N kweli elimu juu ya uongoz hasa jamii n muhimu Sana hili nalimudu nishaongoza na kuwakilisha nafasi mbalimbali Ila sio kisiasa

2. Hapa n busara na hekima za mtu husika Kwan watu wanatabia na maono tofauti na ili ufike pazuri unajitaji kutumia masikio mawili na mdomo mmoja.

3. N vyema kwenye cabinet ya uongoz lazima kuwe na wawakilishi lakini hili muwakilishi n mmoja tuu pia kabla ya mbunge Kuna diwani na wenyeviti wa mitaa Hawa wote ndio wanakamilisha maana sahihi ya muwakilishi hvyo tutatumia watu Hawa kuwasikiliza na kutusemea pale tunapoona hatuwez kufika, pia wawakilishi wastaafu n muhimu kusikiliza maono yao ili kujijenga vizuri.

4. Hili Jambo kotekote linamaana unaweza kusema ndio au hapana Ila hapa tunaenda kujenga hoja na kutunga Sheria, na kuishawishi serikali kutuletea maendeleo na pia kuishawishi na kuonyesha njia kwenye jamii yetu ili kufika malengo
 
aldeo,
We uonavyo kuna kijana gani aliyeingia ktk siasa za Tz akaonyesha ukomavu wa fikra? Nchi zetu, vijana bado ni watu wa kuwaza jinsi ya kwenda US, Kuvaa milegezo, kushinda bar wakiangalia timu za ulaya, whatsapp kubadilishana pich za ngono, na mengine ya aina hiyo.

Kumbuka hapo hakuna sifa yoyote ya kupenda kusoma. Hata ukiwa kwenye bus au ndege, wote ni kuangalia simu na hutamuona hata mmoja akijisomea kitabu. Akili imedumaa.

Walioingia siasa wakiwa vjana ndo akina Zitto, Mnyika aliyegoma hata kwenda shule, Mdee anayehisiwa kuvuta mimea fulani, Januari aliyeshindwa kushika hata wizara kwa elimu duni na sifaa nyiiingi! nani mwingine kijana?
 
Patriot,
Naamini kwenye kujenga hoja za kuhimiza mtu mmoja mmoja kushiriki katika shughuli za kimaendeleo hao uliwataja waliingia kwa intension flan ndio Mana huwaoni wakideliver what community inahitaji na wàmebaki kwenye maslai binafsi nasio taifa kiujumla.

Amini kuhusu Mimi ninamtizamo wa kubadilisha fikra za vijana na Tanzania kiujumla na amini nitafanikiwa na taifa litajivunia uwepo wangu.

Vijana wenye vision nzuri tupo sema n wachache Sana Ila Mambo ya kujisomea vitabu halianzi tuu hvhv Bali Lina misingi yake na n Hobie pia
 
Patriot,
Kwa maelezo yako wewe ni bibi tena bibi kzee aliyekwisha vunjika mgongo na ni mchawi kuliko wachawi wenyewe huna hata element moja ya kuwa kijana kwani mchango uloutoa hauna tofauti na ile michango watowayo wachawi katika vikao vya ulozi.
 
Kwa maelezo yako wewe ni bibi tena bibi kzee aliyekwisha vunjika mgongo na ni mchawi kuliko wachawi wenyewe huna hata element moja ya kuwa kijana kwani mchango uloutoa hauna tofauti na ile michango watowayo wachawi katika vikao vya ulozi.
Unadhani Busara na uelewa ni jambo la kuombewa? Hata useme mema namna gani, bado vijana watashinda kwenye TV wakisubilia Mbwana Samata. Uelewa ni duni na umekwisha fika hadi miaka 40. Kuna watu wana miaka 55 nao unawakuta wanakoroma kuhusu ligi ya UK. wabunge nao wamegundua ni kizazi cha michezo tu bila fikra, wanakuanzishia ligi ili uwape kura. Bure kabisaaa!

Komaeni lakini uelewa uko chini sana! Hata graduate, hana kitu kichwani!
 
Unadhani Busara na uelewa ni jambo la kuombewa? Hata useme mema namna gani, bado vijana watashinda kwenye TV wakisubilia Mbwana Samata. Uelewa ni duni na umekwisha fika hadi miaka 40. Kuna watu wana miaka 55 nao unawakuta wanakoroma kuhusu ligi ya UK. wabunge nao wamegundua ni kizazi cha michezo tu bila fikra, wanakuanzishia ligi ili uwape kura. Bure kabisaaa!

Komaeni lakini uelewa uko chini sana! Hata graduate, hana kitu kichwani!


Naona umeegemea kwenye upande mmoja wa vijana wasiojielewa vipi unadhani Tanzania hakuna vijana wasio jielewa?

Mtu mwenye 45years so NI bado kijana?

Kushabikia Mpira n mapenzi ya mtu, Kuna mwingine kulala, mwingine ulevi, mwingine ibada, mwingine uzinzi, Yan n kitu ambacho kipo na unacho lakin sio Kaz yako ya kwanza
 
Naona umeegemea kwenye upande mmoja wa vijana wasiojielewa vipi unadhani Tanzania hakuna vijana wasio jielewa?

Mtu mwenye 45years so NI bado kijana?

Kushabikia Mpira n mapenzi ya mtu, Kuna mwingine kulala, mwingine ulevi, mwingine ibada, mwingine uzinzi, Yan n kitu ambacho kipo na unacho lakin sio Kaz yako ya kwanza
Boss, tunajadili uzembe na mtu kutaka kuhamasisha vijana. Unayoyataja; mpira uzinzi, ulevi, nk. ni entertainments. Kama hayo unayaona ni primary ujue akili bado haikuruhusu kuongoza wengine. Tuhamasishe watu wanaojitambua, siyo vijana.

Mchakato wa 2015 ulianza na hadithi kama hii matokeo yake CCM ikajaza watu zaidi ya 60 wote wakitaka kuwa marais. Walioenda mbele nikama huyo Januari akijiita kijana. Akapewa wizara, nini alichokifanya? Ukishaona mtu ana miaka 60 anajiita rais kijana, bado anawaza disko na kusafiri saana badala ya jukumu la uongozi, ujue ni malezi duni ktk jamii. Ukilogwa kumchukuwa wa miaka 30 hapo ndo utajikuta unaingiza mtu anayeshinda kwenye mashindanió ya urembo.
 
Patriot,

Aisee naona hii n ngoma ngumu lakin amini wapo vijana wazur wanaweza kujenga hoja kutoa fikra chanya katika kutatua matatizo ya jamii husika pia Kuna vitu vingine haviitaji akili kubwa ili kubifanikisha vingine n power tuu, vingine n uelewa tuu, vingine n kusema tuu
 
TAIFA LENYE VIJANA WAPUMBAVU.

"Mwalimu Nyerere aliwahi kusema katika taifa tunahitaji kuona vijana Jeuri, Wenye kukosoa na kuonya Miiko na maadili katika Jamii sio akina ndiyo mzee"

ndio mzee ni akina....
1.JINGA LAO.
2.KAWE ALMNI.
3.CRIMEA.
4.YEHODAYA.
5.USSR.

Tena mwalimu aliendelea kusema ni upumbavu na ujinga kuwa na jeshi kubwa lenye silaha nzito bila kuwa na vijana katika nchi.
 
Back
Top Bottom