MR TOXIC
Senior Member
- Jun 4, 2019
- 190
- 525
Habari vijana wenzangu wa JF. Nimeona nije hapa nizungumze jambo moja kwa ufupi sana.
Nadhani mnafahamu fika mchuano uliopo kati yetu na wazee wetu hasa tunapokuja kwenye suala la kujinyakulia vigori. Ni dhahiri shahiri tumezidiwa kete kama siyo kupotezwa kabisa maana wenzetu wamejipanga kweli kweli na wanazidi kutupiga bao siku hadi siku.
Sasa niwaombe vijana wenzangu tutafute pesa kujiimarisha kiuchumi ndio mwarobaini wa hili tatizo. Kama tukizubaa basi tutarajie kupigwa chenga nyingi za mwili na magoli ya visigino kama inavyoonekana hapa pichani